MAISHA YENYE FURAHA NA AMANI KATIKA NDOA.
MHUBIRI 9: 7-9
“Enenda zako ule chakula chako kwa FURAHA unywe Mvinyo yako kwa moyo wa KUCHANGAMKA kwa kuwa Mungu amekwisha kukubali kazi zako mavazi yako yawe meupe siku zote na kichwa chako kisikose MARHAMU.
UISHI KWA FURAHA NA MKE UMPENDAYE SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO- ya ubatili ulizopewa chini ya jua…………….
-Nyumba na mali ni URITHI apatao mtu kwa babaye – BALI MKE mwenye BUSARA… MTU- hupewa na Bwana Mith 19:14.
-Kila Mwanamke mwenye Busara hekima hujenga Mith 14:1
-Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima. Mith. 11:16 Mwanamke mwema ni taji ya
Mumewe Mith 12:4.
-Mke mwema kima chake chapita LULU SAFI –chapita utajiri wote wa Marekani na
Japani Mith 31:10.
-MUME wa MKE hujulikana popote kwa ajili ya mke wako Mith 31: 23.
-Nawe umfurahie mke wa ujana wako ni ayala apendaye na paa apendezaye maziwa yake yakutosha siku zoke. Na upendo wake uushangilie daima Mith. 5:18-19.
-‘Na tamaa yako itakuwa kwa mume wako naye (atakuongoza) atakutawala”. Mw. 3:16.
-Ya kwamba kila mwanamume ATAWALE nyumbani mwake Esta 1:22.
-Simpi ruhusa mwanamke KUMTAWALA. MWANAUME ITIM. 2:12 Ef. 5:22.
TAFADHARI: Mith 1:3-5
-Kijana PATA BUSARA itakayokulinda siku zote za maisha yako na UFAHAMU utakaokuifadhi kila siku mafundisho haya katika maisha yako ya ndoa wewe na mkeo yatakuwa:-
i. Wokovu kwako –kukuokoa usifuate njia za waovu.
ii. Yatakuokoa na mambo ya watu wanenao mambo yaliyopotoka-utayajua
yaliyonyooka. Zab.119;105.
iii. Yatakuokoa na watu waziachao njia za Giza.
iv Yatakulinda na watu wanawanafurahia kutenda mabaya.
v. Yatakuhifadhi na watu waliotoka katika njia zao. Watu wakaidi katika mapito yao.
vi. Yatakuokoana Mwanamke Malaya atakayetaka kukupata kwa UBEMBELEZI wa maneno yake.
vii. Yatakuokoa na watu wale waliosahau agano la ndoa zao.
Watu waliosahau Agano la Mungu La Ndoa.
a) Nyumba zao zinaelekea mauti
b) Mapito yao yanaelekea kwa wfu (kuzimu).
KAMA UKIAMBATANA NA WATU WA JINSIA HII NDOA YAKO NAFSI YAKO UZIMA WAKO VYOTE PAMOJA NA WEWE MTAANGAMIA. (MITH 3:1-4).
KIJANA YASHIKE MAFUNDISHO HAYA KWA MOYO WAKO. UYAANDIKE KATIKA KIBAO CHA MOYO WAKO NA HESHIMA
(katika ndoa yako)
MAANA KAMILI YA KUMPA KIJANAMAONYO HAYA:Mith. 21:20.
a)Ni ili kijana / binti apate kuenenda katika njia za watu walio wema.(katika ndoa yako) Mith. 21:20-mwanangu wabaya wakikushawishi wewe usikubali) mith 1:10.
(b) Kuna ndoa za waovu na ndoa za wenye haki. Tunalenga kija na ayashike mapito ya wenye haki.katika ndoa yake.
(a)Maisha ya ndoa yawe na UNYOFU na UKAMILIFU-ili ndoa yenu iweze kudumu hapa ulimwenguni. (ndoa zenye hila zitang’olewa.)
MATUMIZI YA ULIMI KATIKA NDOA YAKO KIJANA - NDOA NYINGI SANA ZIMEFAULU AU KUHARIBIKIWA KWA MATUMIZI MAZURI AU MABAYA YA ULIMI.
HEBU TUANGALIE KATIKA MAANDIKO ULIMI UNA NINI ?
1. Wimbo 4:11 – Bwana Arusi – midomo yako itadondoza asali (maneno matamu) tena chini ya ulimi wako kuna maziwa na asali. NI UAMUZI WAKO KUTOA VITU VILIWE NA BIBI ARUSI WAKO.
2. Bwana Arusi –uzima, afya, njema, amni, mafanikio, baraka, neema, uhai- vipo chini ya ULIMI WAKO.UTUMIE VIZURI ili uiponye ndoa yako na mkeo aule- ulimi wako –apate AFYA NJEMA YA ULIMI) Mith 18:21.
3. KIJANA UTAKULA MATUNDA YA ULIMI WAKO UKINENA JEURI UTAVUNA JEURI –UKINENA UZIMA UTAPATA UZIMA.USITARAJIE KUNENA OVYO-UJIBIWE WEMA, USIMLAANI BIBI ARUSI WAKO USILETE MAUTI KATKA NDOA YAKO KWA ULIMI WAKO. KUMBUKA:Ukinena unapanda ngojea mavuno.
4. KIJANA –UWE MKAMILIFU –ULINDE-
Usijikwae kwa ulimi wako Yak. 3:212 ulimi ni moto.Ulimi ni ule ulimwengu wa uovu. Ulimi utautia au utaitia ndoa yako unajisi –ULIMI: Utawasha moto maumbile yote ya Ndoa yako njema nautayaharibu.
ULIMI:UNACHOCHEWA NA KUZIMU- Ni kiungo chenye msukumo na JEHANAMU.
ULIMI: HUJIVUNA, HUJIINUA, HUJITUKUZA kwa MAJIVUNO makuu mno.
ULIMI: Ni uovu usiotulia - YESU tu anaufunga.
ULIMI: Umejaa sumu iletayo mauti. Bwana Arusi: Panga ni jema ukitumia kwa matumizi mema. Na ULIMI ni mzuri ukiutumia kwa vizuri.
ULIMI: Ni mzuri kwa wale wautumiao vizuri na wanafurahia matunda yake.
ULIMI: Kwa mtu mbaya katika moyo wake anatoa mambo mabaya. Mt. 121:34-35- kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.
ULIMI:Utayatambulisha yaliyoko katika moyo wako.
ULIMI: Unaweza ukautumia vyema ukatoamaji matamu yenye uzima. Yoh. 4:14.
ILIMI:Unaweza ukaazimu ukatoa maji machungu.
ULIMI: Maneno yake nikama maji ya vilindi kijito kibubujikacho chemchem ya hekima.
ULIMI: Huita mapigo, huita mikosi, huita balaa, huita umaskini.
ILIMI: Utaangukia msiba ukiwa na ulimi mpotofu. Mith 17: 20.
ULIMI: Huchochea magumu mith 15:18, mith 17:14, acheni ugomvi kabla haujafurika.
TUMIA ULIMI WAKO VIZURI : Mith
Usiwe mkorofi- ukamvunja mkeo ulimi wako tu. Uwe na ulimi safi ili NDOA YAKO IWE NA UZIMA – uwepo uzima katika nyumba yako.
FIKIRI UTAKAVYOMJIBU MKEO
Moyo –ndio wenye hazina ya maamuzi yote – ulimi hunena tu pale moyo unaporuhusu unene.- ULIMI mzuri maneno yapendezayo ni zaidi ya asali ya nyuki. Utamu wake tiba yake afya yake, tena huleta utamu hadi nafsini mwa mkeo. – tena utampa kunenepa na afya mifupani. Mith. 16:13.
SEMA MANENO YALIYO SAWA.
Ili yalete furaha katika ndoa yako tena yatakufanya upendwe na mfalme- malkia.
UTAMU WA MANENO.- huongeza ELIMU 16:21- Maneno yatakupa uelimike zaidi. Maneno ya ilimi huleta hasara tu.
UWE NA ULIMI MPOLE. Ulimi huo hugeuza GHADHABU - epuka - maneno yaenezayo TAMKA maneno yenye maarifa vizuri. JILINDE: Usimwage Upumbavu, Mith 10: 19- Penye mengi hapakosi ULIMI. Ni Mith 12: 18- afya. UWE NA MIDOMO YA KWELI ILI UTHIBITISHWE USIWE NA MIDOMO YA UONGO.: Mith 12:25. UWE NAMANENO MEMA: Mith. 12 :25 neno jema huufurahisha moyo kunena maneno mengi ni upumbavu. Mith 10:8.
MDOMO- hulisha wengi 10:21 ya mwenye haki.
ULIMI NI FEDHA TEULE- Utumie kuleta faida. 10:20 Nena maneno yanayokubalika. 10: 32 ULIMI wa ukaidi utakataliwa mbali kinywa chako – kiwe ni cha mwenye haki.
BWANA ARUSI: Ukitaka kuona kila siku ni njema , zuia ulimi wako usinene mabaya, na uangalia sana kinywa chako kisinene hila. 1Pet 3:10.
UWE MWANAMUME ANAYENENA MANENO YA IMANI TU.-USIWE MTU WA WASIWASI MTU WA KUSEMA MASHAKA , MTU USIYE TUMAINIKA JAA IMANI NA ROHO MTAKATIFU,UWE MUNGU KATIKA NYUMBA YAKO , MUNGU AONEKANE KWAKO.
KAA NA MKE WAKO KWA AKILI.
Sheria yua mwenye akili.-ni chemchem ya uzima. (1 Pet 3:7-8).Enyi waume kaeni na wake zenu kwa akili.
BWANA ARUSI: Kukaa na mke si pesa wala mali, wala kiroho bali inahitajika akili. Tito 2:1-4 Wazee wa kike wawe na mwenendo mtakatifu. Wawe wanafundisha mema. Ili wawatilie wanawake vijana AKILI ili wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao, na kuwa na kiasi , kuwa safi kufanya kazi za nyumbani na kuwatii waume zao kuwastahi. Ef 5: 33. kama wazee wa kike watawtilia wasichana akili za kuwa wake wema kadhalika na wazee wa kiume watatilia vijana wa kiume akili ya,
i. Atalishika neon la Bwana bila KULISAHAU.
ii. Tena azishike amri za Bwana kwa moyo.
iii. Njia yako kijana itakuwa safi kama utasikia neon la Bwana na kulitii, zab. 119:9, mith 3:1-4.
AKILI ZAKO.
KIJANA : Kuna akili ya kwa kwako mwenyewe ya kuzaliwa na kuna akili ya kutiliwa na walimu, wazazi na walezi. Lk.1:17. KUMTILIA MTU MWASI AKILI YA MWENYE HAKI. Usizitegemee akili zako mwenyewe, kuna kumtilia kijana akili zawatu walio na wake ili ajue kumchukulia mkewe kwa ufahamu kamili. Mit. 3:5-6.
AKILI NZURI:
KIJANA: Utapata akili kwa kufundishwa na kuyasikiliza ya baba zako, wachungaji wazee mbalimbali, walezi, n.k. Mith 4:1 mama naye anamfundisha mwanae wa kiume Mith. 4:3, 31:1, Mfalme LEMUEL aliusiwa na mama yake wamama wanasehemu kubwasana katika kuwafundisha vijana wa kiume.
AKILI YA MOYONI: Kijana uwe na akili ya moyoni mith 10:8 kuna akili ya mambo ya dunia hii na kuna akili ya moyoni ya kumtafuta Bwana kwa hiyo kuishika mafundisho kunampa mtu AKILI NJEMA kuyaweka akiba mafundisho na amri za Bwana. Mith 7:1-5
KIJANA MWENYE AKILI: Mith 6:32
i. Hatakubali kufanya uzinzi milele.
ii. Hatakubaliana na ubembelezi wa mwanamke Malaya mith 7:5.
iii. Kijana tumia kabisa akili yako usiwe na mazungumzo mabaya kwani yanaharibu tabia njema.
iv. Kijana mwenye akili –Mith 7:5. hatakubali kamwe unafiki na Malaya.
KIJANA ASIYEKUWA NA AKILI
a. Atamwacha mke wake atakimbilia wengine – tamaa. Mith 6:32.
b. Mwanamke mzinzi atamkuta na kumbusu.
c. Atashindwa na ushawishi wa kahaba na ulaini wa maneno ya kinywa chake na ubembelezi wa midomo.
d. Ataingia kwenye uzinzi amsahau mke wa ujana wake. Mith.7:22.
e. Atapata hasara ya nafsi yake.
f. Aende nyumbani ambayo ni njia ya kuzimu mith 7:22-27.
g. Aishukia mauti akiwa anaangalia mith 6:33.
h. Kuingia katika unzinzi ni kuvunjiwa heshima na kujipatia fedheha isiyofutika milele.
UWE NA KIASI.
Kijana katika ndoa wewe na mke wako mambo yenu yote yatendeke katika uzuri na utakatifu.
Eb. 13:4. NDOA YENU MUIHESHIMU ninyi wenyewe wanandoa. Na imeandikwa malazi yawe safi.
i.
j. ANGALIA SANA:
Mnapoona mko pamoja meza moja usiwe mbinafsi sana ukamsahau unayekula naye.
ii.ANGALIA SANA.
Usiwe mtu mbinafsi na kuiacha sahani bila chakula. Ukimwacha mwenzio njaa
analala anahangaika bila raha.
iii. CHUNGA SANA:
Mue mkeo mjali mpe mlo ule anaoutaka usimnyime iliyo haki yake mpe hake
sikia anavyotaka mwenzio na umtimizie usiwe na amri juu ya mwili wako
mwenyewe. 1kor 7:2-5 wewe ni mdau mkubwa wa tendo la ndoa ndiwe ile
chemchem ya baraka. Mith. 5:15-19 vijita vyako vinaufurahisha mji wa malkia
wako kumbuka kila jambo lina wakati wake mwache mwenye chake atumie kama
apendavyo –usimpe kama utakavyo.
iv. ANGALIA ASALI NI NJEMA SANA LAKINI;
HAIFAI KULA MNO.
Kula kiasi cha shibe mt. 27:7 angalia Bwana arusi ujue kila mke wako akishiba akasema asante kwa chakula usimlazimishe matonge zaidi maana atavimbiwa, alichotangulia kula acha shibe ya leo iwe hiyo hiyo ujue shibe ya sasa ni njaa ijayo, mtu akishiba ananawa akiachwa katika hali ya furaha yake hivyo atakupenda na kesho akiwa na njaa atakuambia nawe zingatia mtangulize mwenzio. JE UNAJUA KWAMBA MCHELE NI MMOJA LAKINI MAPISHI NI MBALIMBALI?” Bwana arusi wmache bibie akupikie mapishi yale anayoyajua, mpe uhuru akukaangizie mapishi yote kasha kama wewe umeenda shule na umekula kitabu vizuri ukamaliza vidato, hata ukafikia mlimani hapo sasa mweleze mwenziotaratibu kidato hadi kidato kwa hekima na taadhima ukimpeleka taratibu katika madarasa hayo hatimaye atahitimu vidato vyako na kesho ataanza kukupikia cile citu unavyotaka hadi chuo kikuu atakupa kile utakacho. Hatimaye matajiri na wasomi wa hali ya juu sasa mnapoamua kula mtakuwa na meza kubwa yenye vikorombwezo vyote sio msosi wa shida ugali, tembelea ti au wali dagaa tu na viazi maharage basi kila siku ni hicho hicho, hata nyama kila siku inakinaisha kuleni katika meza kubwa JUENI KUBADILI MLO KILA MNAPOLITAKA GHALALI MWENU MBAVINGI VITUMIENI WEKENI MBOGA ZOTE MEZANI MTU CHAGUE KULA KIDOGO KIDOGO kila kitu hata asikie kushiba bila kujua kashiba nini.
v. ANGALIA USIWE MWEPESI WA HASIRA:
Mh. 7:9 mwepesi wa hasira ni yule anayeiweka hasira kifuani mwake uwe mwepesi wa kusikia tawala roho yako mith. 16:32 usiwe mwepesi wa kusema au kukasirika yale 1: 19 -20 hasara ya mtu haitendi haki ya Mungu.
Vi. ANGALIA SANA USIWE MTU WA MANENO MENGI:
Kumbuka somo la ulimi kwamba penye maneno mengi hapakosi kuwepo na maovu.
i) Maneno yako yawe machache lakini yape hekima na busara.
ii) Maneno yawe mazuri yafae Neema tena yamfae kila anayesikia Kol. 4:6.
iii) Nena kwa wakati wake dondoza asali hata mkeo atamani uongee tu.
iv) Neno ovu lisitoke kinywani mwako. Ef. 4:29.
v) Toa majibu sahihi na uyasimamie 11kor. 1:18-20.
Vii USIWE MKIMYA MNO.
- Mtu wa kukaa kima bila sababu ni mzuri lakini kima kingi kina kishindo.
- Kunahitajika maziwa na asali utawanyima haki yao .
- Mambo yote yatendeke kwa utukutu wa Mungu usikae kimnya umzimishe roho.
- Mfurahishe mkeo kwa ma neon ya kinywa chako.
- Bora uwanunie wote lakini kijito cha baraka cvha maziwa na asali akiona mpenzi wako wa moyo siku zote.
viii. USIWE MTU WA KUJIAMINI SANA.
1. Unaishi na mwenzi wako maamuzi yako yaweke wazi upate ushauri.
2. Elewa kwamba mko na mwenzako ukikosea katika jambo lolote linawaathiri wote acha ulicho nacho wengine wakiamini usije ukaangamia bila wa kuponya.
ix. ANGALIA USIWE MCHOYO KUPITA KIASI;
Uchoyo ni roho ya kuwanyima watu haja zao wanazozitaka kwao.
a). Uwe mkarimu kwa yale yote yapasayo kukirimu.
b) Usiwe mchoyo hata chumvi kwa jirani mpaka baba kulizwa
c). Uwe na ukarimu kiasi na uwe na hekima katika jambo hili.
x. USIWE NA WIVU KUPITA KIASI
a). Kama mume mzuri lazima uwe na wivu kwa mke wako lakini uwe na kiasi.
b) Si wivu wa kumzuia mkeo kucheka na mtu au akisalimiwa njiani na mtu tayari maswali huyu ni nani na mlijuana lini? N.k.
c). Mwamini mkeo mpe raha mwambie yale unayopenda mpe nafasi akuambie naye ayapendayo wekeni mambo sawa.
xi. ANGALIA USIWASAHAU WAZAZI NA JAAMA.
-Kkuna wazazi wako na wazazi wa pande mbili. ( kwa mke wako).
W amekupa binti yao usiwape kisogo binti huyo bado ni motto wa wengine wajali uwahudumie ili mwenzio akupende.
- Jali pia wale wazazi waliokuzaa wape ukarimu na fadhili kama walivyokutendea wewe usiwasahau usiwafanye wawe ombaomba kwako. Pata baraka zao kwa kuwatunza.
xii. USIMSAHAU MUNGU WAKO ALIYEKUUMBA.
§ Ndoa ni kanisa la kwanza wewe na mkeo jengeni msingi wa maombi na kumtanguliza Bwana.
§ Mtolee Mungu fungu lake ili nyumba yenu ijae Mungu aibarikie kazi ya mikono yenu.
§ Someni neon la Mungu daima wewe na mke wako litafakarini neon usiku na mchana. Zab. 1: 1-6.
§ Iwe ni amani ninyi kwa ninyi iweni na utakatifu katika mwenendo wenu wote kila siku.
§ Kaeni ndani ya Yesu tembea na Bwana daima dumu ndani ya Yesu ongozwa na Bwana usiku na mchana. 1nyak 28: 9, kumb. 6: 4-8.
WAJIBU WAKO KAMA MTU MUME.
1. Wewe ni mwanaume.
2. Wewe ni mume.
3. Wewe ni baba.
1. WEWE NI MWANAUME.
-Una mfano wa Mungu.
-Una sura ya Mungu.
- Umepewa kutawala.
2. WEWE NI MUME.
-Una mke utampa haki yake kama ipasavyo mume.
- Utakuwa mme wa mke mmoja.
-Utakaa katika nafasi yako kama mume ukimlinda mkeo awe wako tu.
3. WEWE NI BABA.
-Utabarikiwa kuwa na watoto.
-Utawalea katika hicho cha Bwana.
-Utawapa urithi wao kama Baba.
- SI VEMA MTU AKAE PEKE YAKE- mw 2;18.
- NITAMTENGENEZEA MWENZAKE WANAYELANDANA: M. 2:18.
1. Nyama – KHc NYAMA ZAKE.
2. NI MIFUPA KATIKA MIFUPA YAKE.
3. SI NGOZI KATIKA NGOZI YAKE (ngozi inapendeza inavutia- laini)
- USINGIZI MZITO NI NINI?
- Mungu anakushughulikia.
- Kutana na uwepo wa Mungu.
- Kuondolewa ubinafsi.
- Nafasi ya wazi utupu ya mwanaume.
- Faraja – matulizo ya kwanza kuhurumiwa- kupendwa kuheshimiwa kujaliwa kuhudumiwa- kutunzwa.
NI LAZIMA KITOKE KITU NDANI YAKE YA MWILI WA MTU MUME – KITAKACHOKUWA KAMA MFUPA KATIKA MWANAMKE NA NYAMA KATIKA MKE WAKO (PENDO ZITO, KUMHUDUMIA, JALI ). MFUPA – NI FRAME ( NYAMA:- SHAPE – UMBO).
4. KUJIPATIA MKE UMTAKAYE:
1. MTU ANAPANGA – Sifa za mke huyo.
2. Hali ya mke huyo
- Umbo Lake Liweje
2. MUNGU HAPEWI KIPAI MBELE.
- Mtu haombi Mungu amchagulie.
- Mtu hamsikilizi Mungu.
- Mtu haanzi na kuwa na Mungu kwanza – uwepo ushirika na Mungu haupo.
- Hapati uchungu wala maumivu mke ndani ya mtu.
-YULE SI NYAMA KATIKA NYAMA WALA MFUPA WAKO.
- HAMFANANI UNDANI WENU.
- UPENDO USIO WAKUHURUMIANA.
-UPENDO USIO WA KUJALIANA.
- HAUNA HESHIMA WALA ADABU.
- MAPENZI YENYE SABABU.
5. KUNA MTU KUJITWALIA WAKE ESAU- MW 28: 8-9, 36: 2-3, 6.
6. WAZAZI MAKINI – WANAWAPA WATOTO WAO USHAURI KUHUSU MKE.
MW 28:1-6
MW 24: 7 Selective Special family
KUMB 7:2-3
7. MUNGU ANATUMA MALAIKA MBELE ZAKO ILI AKULATE – YULE
UNAYEMTAKA.
a) Bwana anawatuma malaika zake kwa ajili ya jambo hili.
b) Anayekwenda kwa kumtanguliza MUNGU hatangitangi, hagongi mwamba – hadhani dhani – (anadumu katika kumhakikisha Mungu)
c) Atakapokuwa katika vita bado Mungu atakuwa ni KIONGOZI wake (atamtaka Mungu naye Mungu atamdhibitisha).
d) Ataomba lolote – Ishara ya kumjilisha na Mungu atamdhibitishia. Haitatokea ishara yenye utata.
e) Yue Mungu aliyekuchagulia – Anasura nzuri ni mkamilifu mbele zako hata wewe UTAMPENDA.
f) Yule uliyemtaka kwa Bwana – Ishara ile ile uliyoiomba itatakia kwake.
g) Unatakiwa UMKAZIE MACHO – UNYAMAZE (UONE) UJUE KWAMBA BWANA amekufanikisha au sivyo.
h) Mrudishie Mungu utukufu – utakapoona msujudia Mungu- Mshukuru tu Mungu.mkumbuke aliyekuongoza – ataimaliza hiyo kazi njema- ataimaliza.
- JIHADHARI – USIDHANI UPAKO UTAKUZUIA KAMA HUTALISHIKA NENO LA MUNGU SAMSON –KMB. 7: 3- 4-USIMWOE ASIYEMCHA MUNGU WAKO (MFANANE KIROHO)
-Ukizoelea –utapata maono ya huko- huko.
-Macho hayana jibu – wala kukubali kwa yule kijana au binti si jawabu.
- 2samw 11:2- Macho –yana mambo yake, mzuri sana – umbo lake – na
wakupendeza macho- mw. 3:6- anguko – macho yanayotamanisha yanayofaa.
- Uwe mwaminifu – kum 22:14 usifanye ukahaba ukiwa nyumbani mwa baba yako- v. 20-21.
- Usionje mboga jikoni (usile( usianze kula
- Kuonja ndoa hakupo –ukijaribu utashawishika.
- Utajialalisha kula – na hutaweza kujizuia.
- Binti wa kuhani akifanya ukahaba – law. 21:9 “MTOENI ATEKETEZWE. “MW. 38:24.
A. Makabila mengi hapa Tanzania na pande nyingi za ulimwenguwa mila na desturi zao katika suala zima la vijana wao katika jamii zao.
KM. WAMAKONDE, WABARABAIG, WAFIPA N.K Bado mpaka sasa mila na
desturi za zina nguvu sana katika jamii yao.
B. Walikuwa na walimu wa unyago kwa mabinti – walioitwa MAKUNGWI) na wanaume walikuwa na wale walezi wao wa jando. (Wazee rasmi katika jamii wateule kuwashauri vijana na kuwafunza mambo yote ya jamii hata ndoa.
C. Wazngu waarabu walipoingia hapa nchini waliingiza taratibu na mila zetu zikaanza kupuuzwa tangu zile nzuri hadi zile mbaya. Lakini tunapaswa tujue utamaduni wetu si mbovu wote kabisa hapana. Yapo mambo ambayo ni lazima tuyazingatie katika utamaduni wetu na kuyageuza yaende na wakati tulio nao. K.M. Mhari yalikuwa ni wanyama sasa tumeyamodfy kuwa pesa.
TOHARA YA KIENYEJI: Sasa tunatumia hospitali njia ambayo ni salama na bora zaidi.
UZAZI WA MAJIRA WA ZAMANI:
Mke anakaa mbali na mume kwa muda mrefu lililopelekea wanaume kuoa wake 2 au 3 kwa kujitosheleza – lakini sasa tuna njia bora za uzazi – ni kuwaona washauri hospitalini.
SHEREHE ZA HARUSI ZA VILEO.
Zamani starehe yao ilikuwa ni pombe na nyama – lakini leo tuna tuna mabadiliko – tunatumia soda na chakula vitu vya gharama ndogo tu.
NGOMA YA ASILI:
Ilikuwepo sasa – kuna mziki wa vyombo, DJ, Matarumbeta na NCC.
MADARASA YA JANDO NA UNYAGO:
Sisi leo tuimarishe darasa hili la kitchen party kila kabila au jamii walihusika sana kuwaeridhisha vijana wao utamaduni wa kabila lao- hata mila na desturi za kabila lile walifundishwa wazijue.
MAFUNDISHO YA TABLE/ KITCHEN PARTY – YANAFAIDA GANI KWA VIJANA (KE/ME) ?
1. KUMPA KIJANA NDOA NZURI YENYE,
a) Raha – kila siku.
b) Furaha – daima
c) Mafanikio ya maisha yao yote. (Mika 4:6)
11. KUMUEPUSHA KIJANA NA MAKOSA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA KWA KUMPA TAHADHARINA MIFANO
BORA YA KUISHI NA MKEWE (MIT 1:4.)
111. KUELIMISHA KIJAN WA KIUME/KIKE AJUE KUISHI NA
MKE/ MUMEWE (BILA UGOMVI, AU MAFARAKANO
AU MATENGANO AU CHUKI) MALAKI 2:14-16 KUMPA
KIJANA URITHI WA HEKIMA. MW. 7:11.
1V. KIJANA KUMUONYESHEA HEKIMA YA JINSI YA
KUISHI NA MKE WAKE – TENA KUMPA KIJANA
UFAHAMU – WA NDOA ILI AISHI KWA UHERI SIKU
ZOTE ZA MAISHA YAKO NA MKE WAKO
AMPENDAYE MITH. 5:18-19.
V. Kumwelimisha na jinsi atakavyomfurahia mkewe.
- Na kutosheka na mke wake
- Na kuushangilia- Upendo wake daima (ni nini?) kuwasaidia vijana.
A. Waongezee wingi wa siku zao.
B. Watajirike kwa ajili ya Bwana.
C. Njia (maisha) ya kupendeza wawe nayo.
D. Wawe na amani siku zao zote.
VI. KUMWEKA KIJANA ACCOUNT YA MAARIFA; akiba ya siku
zijazo mith. 2:1-2. Ef. 6:23. Kijana awe amevaa silaha zote- ili
aweze kusimama siku ya uovu.
VI. KUMPA KIJANA NURU NA MWANGA WA KULE AENDAKO – MAELEZO YA MAISHA – ZAB.119:9;130
KASORO ZINAZOJITOKEZA SASA KATIKA KITCHEN PART
1. Jambo linaweza likaanza kwa maana nzuri lakini baada ya muda Fulani watu wengine wakaanza kulipotosha maana halisi ya jambo hilo.
2. Yanapoanza kuongezewa vitu Fulani Fulani mambo haya kitchen part kama sare za wanamama wote, ukumbi wa kifahari, kumremba mwanadada kwa gharama nyingi, sherehe kubwa kama ya harusi – basi yale mambo ya adili huwekwa kando kabisa km.
i. Binti hapewi muda mrefu wa mafundisho
ii. Muda wa walimu unakuwa mdogo mno km (30min; 20min; 60; 90min).
iii. Walimu makini wazoefu wajuzi wa mambo ya ndoa – ni wachache.
iv. Ingefaa uwepo – muhtasari maalum kijana/bint ayajue – kuanzi – siku ya harusi, hadi uzeeni.
v. Ingefaa – tuwe na mambo muhimu ya kuwaasa vijana na mabinti – ili huyu akiandaliwa katika msimamo huu na mwingine aandaliwe kwa mtazamo utakaoana na huu wa pili.
vi. Mara nyingi kwa kukosa muda mrefu wa mafunzo – maarusi wanapewa dokezo la maisha ya ndoa na wala hayana upana wowowte. Tena wanampa semina hiyo siku za karibu mno na kufunga harusi wameanza kuwa na shughuli nyingi mno kuliko kawaida wala hawana muda wa kuyatafakari hayo.
vii. Mara nyingi wanandoa wenyewe hawana haja na mafundisho hayo kwani wengi wao wanajua kabisa kuwa ndoa maana na kwamba the whole (perment sex partner) content ya ndoa ni sex.
viii. Wengi wa walimu wanafundisha mapenzi na style zake ili wanandoa wafurahie jambo hilo – lakini mambo mengine kama vile (km)
- Kuheshimu jamii ya mume
- Kutunza kinywa – ukali – kutulia
- Kutumia pamoja katika ndoa
- Kutanya kazi kwa bidii
Tunapendekeza iandaliwe syllabus kamili ya mambo hayo katika kanisa la Mungu iwe kama kiongozi cha mafunzo na mengineyo ufunuo wa Mungu utatenda kazi ndani ya waalimu wenyewe. Kama ndoa zitajengewa msingi imara mambo haya yatajitokeza.
a) Migogoro katika ndoa itapungua
b) Ndoa kuvunjika haitakuwepo kabisa.
c) Ndoa nyingi zitafanikiwa kiroho na kimwili pia na kiuchumi.
d) Manyanyaso katika ndoa yatapungua
e) Watu watatamani kuokoka ili ndoa zao zifanane na ndoa zetu.
MAWAZO YA WACHUNGAJI WA WATUMISHI WENGI KUHUSU NDOA: Zisizo na mafunzo au maelekezo.
a) Hawaoni kama kuna hatari yoyote watu wakioana bila kufundwa kama ilivyo hatari kumwajiri mhasibu asiyesomea uhasibu au kumpa gari dereva asiyejua udereva – ndivyo itakavyokuwa kwa wajinga wawili kumpa ndege mtu asiyerubani.
b) Watumishi wengi hawakupitia darasa hilo la ndoa. Walipewa wake tu na hata ukiwauliza watakuambia lakini hata wiki moja ya mafunzo hawakupata. Ndoa bila mafunzo inadumu hii ndiyo sababu wachungaji wengu hawatilii maanani semina za wanandoa kabla ya kuoana na hata zile za waliooana.
c) YAWEZEKANA PIA – Wachungaji wengi ndoa zao zina matatizo hata hawajui wanaomwambia nani matatizo yao kwa hiyo wanakufa na TAI ZAO shingoni.
d) Yawezekana wachungaji wengi hawana ujuzi wa kufundisha mambo hayo katika makanisa yao ( na haya ni mnayaona sehemu nyingi niizofanya huduma ya vijana au ndoa)
e) INAWEZA ikawa watumishi hao hawajui waanzie wapi au hata hawajui maandiko watakayosimama nayo kutoka katika biblia. Hii ndiyo maana tunataka tutoe kijarida kidogo kitakachotoa mafundisho kamili juu ya KITCHEN AU TABLE PARTY.
f) YAFAA – WAWEPO WATU KATIKA KANISA WENYE MOYO WA KUFUNDISHA HAYO. Na waruhusiwe.Hawa na waongezewe hiki kijarida ili pamoja na ujuzi wao wao walionao wawe na uana zaidi wa kuwaelimisha mabiunti na vijana.
g). YAFAA SANA WALIMU WA KITCHEN PART, Wwakajua mambo yatakayofundishwa kwa vijana – TABLE PARY ili waweze kuboresha somo lao vizuri zaidi kwa mabinti, kadhalika nao waalimu yanayofu dishwa kwa upande wa mabinti ili aweze kumechi somo lake vizuri yasipishane.
MAMBO AMBAYO SI MUHIMU KATIKA KITCHEN AU TABLE PARTY.
1. Sare za wote wanaoshiriki kwa nini msiikusanye hyo hela hata mkamuuliza binti anunuliwe kitu gain cha kumfaa?Wakati mwingine zawadi wanazompa wala hazifiki thamani ya gharama za kukodi ule ukumbi au zile sare zao.
2. Haifai kugharamikia mara mpambaji wa laki 2 na ukumbi wa laki 3 kwani nini hiyo fedha mkaitumia kwa shughuli nyingine ya kumwanzia maisha huyo binti huyo.
3. Matarumbeta mziki wa gharama MC wa kukodi na mantaishashi kupindukia. Kwa nini vitu hivi vichukue uzito wa kwanza tena arusi iwe kama imefungwa mara mbili upande mmoja kufuatana na gharama zisizo na sababu.
4. Ni muhimu sana uwepo muda mrefu wa mafundisho kwa kijana /Binti na mwalimu asiwe mmoja ili aweze kulinganisha ukweli toka mwalimu hadi mwalimu awepo mwanaume mmoja Table party/ au mwanamke mmoja kwenye kitchen party.
5. Binti /Kijana atakapofika kufanyiwa SEND- OFF /Table party awe amehitimu katika jambo hilo siku ya kitchen/table party isiwe ni mwanzo wa darasa bali uwe ni hitimisho la sherehe hizo.
Kutokana na mmomonyoko wa maadili tunaouona katika Taifa letu; Huu
umesababishwa na vijana anafanya yale.
a).Ayaonayo wengine wanafanya ili mradi yanayomfurahisha au auonayo katika TV.
b).Vijana waniga lolote walionalo katika aTV au magazeti ya nchi za nje au Internet.
Wanayaifa hawana msimamo.
c). Maana kamili ya maadili sasa haipo kwani vijana mashuleni hawapewi mafunzo
makamilifu yanayohusu utamaduni wa mtanzania au mwafrika.
Kutokana na kuupuuzwa kwa mila zetu na desturi zetu vijana mbalimbali hawana
Dira, wala utamaduni. Ingefaa idara ya elimu wabuni kijitabu ambacho
kingefundisha mila na desturi ya Mtanzania kitakachobuniwa na jopla wazee wa
busara kutoka makabila mbalimbali hapa nchini ili angalau kitumike mashuleni
kama Dira ya jamii. Ni lazima sisi wa kizazi hiki tuanze kuwaaandalia vizazi
vijavyo.
(a). Usalama wao (kutunza ardhi, hifadhi zetu kpanda misitu n.k).
(b). Chakula chao.
(c). Utamaduni watakaofuata.
(d). Hata mavazi ya kitaifa tuyabuni.
(e). Maadili ya kitaifa tuyabuni.
Makabila yake yote hadi miaka ya 1960 na 1970 kuna wengi bado walikuwa wanajali sana mapokeo ya makabila yao. Sasa Tanzania ni Taifa ukabila wa mtu awaye yote.Tuunde basi mwongozo wa kitaifa ambao utatiwa mkazo sana toka std 1 na katika mashule yote. Km
- Kuvaa nguo za heshima.
- Kusalimia wakubwa.
- Heshima kwa wakubwa.
- Maisha katika jamii
- Utaifa na siasa
- Kufanya kazi kwa bidii
- Ufundi staid na kilimo
- Ufugaji na ajira.
Zipo njia nyingi za kulinda taifa letu na kulinasua kutoka katika mmomonyoko wa maadili. Mojawapo ni hii ya kutumia:
a) Vyombo vyetu vya habari vitangaze mara kwa mara katika vipindi maalumu.
b) Makanisa misikiti wasisitize jambo hilo- pia mabango yabandikwe.
c) Vijarida na magazeti yawe na ukurasa maalumu wa fundisho hili.
d) Viongozi wa siasa wafanye hivyo bado hatujachelewa tunaweza kuokoa
jahazi.
Kanisa linapaswa liwe ni kielelezo cha mambo hayo yote kwa kuweka mipango mizuri ya malezi kwa vijana wao haya ikiwa ni pamoja na mafundisho yaliyosotiwa vizuri kutoka biblia yakionyesha mifano halisi wa neon la Mungu katika maisha ya mteule.
Kanisa lisibakie nyuma kuaanda jinsi ambavyo vijana wake watanashati tena umoja wa viongozi wa makanisa utasababisha mafanikio makubwa ya jambo hili.
Ndani ya Biblia kuna mwongozo wote unaotakiwa kwa maisha ya kila mwanadamu na kama ukichambuliwa vizuri unaweza kufaa si kanisa tu bali jamii nzima ya walimwengu tunaoishi. Binti/ Kijana atakapofika kufanyiwa Send off/ kijana atakapofika awe amehitimu katika jambo hilo- siku ya kitchen party ni mwanzo wa darasa bali uwe ni hitimisho la sherehe.
-