SEMINA ZA NDOA


                                  SEMINA ZA NDOA
            JE NI  NINI HATIMA  YA  NDOA   YAKO?

Utangulizi: PANGA KUMALIZA  VIZURI
Andiko:         Mhubiri  7:7-8
Heri  Mwisho wa neno   kuliko mwanzo wake.
Ndoa   chanzo chake  ni Rohoni.Muasisi  wake ni mungu .Yoh.4:24 Mungu  ni Roho

Tunaishi katika  ndoa  (a)Kwa  Hekima    Mith.14:1
                                     (b)Kwa  Akili        1Pet 3:7
                                     (c)Kwa    Kutii      Efe .5:22-24
                                     (d)Kwa Upendo    Efe .5:25 -29
                                     (e)Kwa  kuheshimiana  Ebr.13:4;1Pet. 3:7b;Efe.5:33b  Staha.

Tena tukumbuke –Mpango halisi  wa mungu kuhusu wanandoa ni  huu:-
            (i) Mke  awe  msaada kwa  mumewe.        Mwa 2 ;18
            (ii)Mume amfurahie mke wa ujana siku zote.Ndoa iwe ni mahali pa furaha  Mhu.9:9  
(iiiMapendo  yawe  ni ya siku zote.Kusiwepo na  kuchukizana –chuki Mith 5:18-19

Ndoa  zetu  tujitaidi ziwe  na
(i)Sifa  njema      Mhu .7:1;2  Kor.6:3-4;Tujipatie sifa njema
(ii)Ndoa    zetu ziwe  mfano mzuri /kielelezo chema kwa
(a)Watoto wetu
(b)Waaminio
(c)Wayahudi  1kor 10;32 1tim .4:12.katika usemi,mwenendo ,imani ,upendo,na usafi .
(d) Wayunani
(e)Maisha  yatu  ya  ndoa kumpa mungu utukufu.1kor.10:31

Tunaweza  kuiga mfano mzuri  wa ndoa  za wazee wetu  kama  adamu, Ibrahimu, Isaka, Nuhu, Ayubu n.k. Ebr.13:7. Walimaliza  vizuri tunaona jamopa na magumu mengi, lakini walikuwa na mwisho mzuri.  Tuiige imani yao.
02. NDOA INA VITATU VYA AWALI.  Ambavyo kila mwanandoa     akivishinda__aandelea mbele kwa ushindi na ndoa hiyo inakua na kumaliza vyema.

KITUTA CHA KWANZA
Kumfahamu mwenzi wako wa ndoa.
Katika KITUTA hiki kunapatikana darasa la kuchukuliana na kuelekezana.
Jambo kubwa katika darasa hili ni wanandoa wote kuwa:-
(a)   Wa kweli kila mtu kwa mwenziwe.

(b)  Wa wazi bila kufichana kitu.
(c)   Wanyenyekevu kila mmoja kwa mwenzake.
Kwenye Eneo hili, mke atumie HEKIMA yake aliyopewa na Mungu Mith. 14:1 na BUSARA Mith. 19 :14.
Kusiwepo na kukosoana wala kudharauliana ama kulaumiana bali uvumilivu na kuelimisha kuwe na nafasi ya kwanza haswa katika HAKI  za mtu katika TENDO la NDOA.  IKor.7:2-5,
Mara nyingi wanaondoa  wachanga  si wastadi   wa TENDO la NDOA maana hawana ujuzi wala uzoefu ; wala hawajui kujizuia au kungojana ili wapate kufikia shibe  ya raha  yao kwa pamoja .

Vile vile hawajui hata namna (style)mbalimbali  za tendo la ndoa ambazo ziko kama 9na 4 maalum ambapo mke ni mjamzito (mgo –solo –mago –ina –wima –kichu –juu –mapa –kuge ,kistu )INAHITAJI  MOYO  WA   UNYENYEKEVU :ili wanandoa hawa wapate kujifnza  na kupata  uzoefu (experience) .Inahitaji  kocha  nao watajipa  uzoefu wao kwa kungojana  na kuchukuliana hadi  waufikie  ujuzi  wa TENDO  la NDOA katika  hali ya kutoshelezana.

Inawezekana mtu kufanya  tendo la  ndoa kwa dakika 5,au 10 au 20au 30 kwa ustadi akamtosheleza mwenzake – lakini inatofautiana mtu na mtu – pia inatofautiana katika maumbile, kwa mfano:-
-       Wanawake wanene wana namna yao na kiwango chao mpaka wafikie kutosheka
-       Wanawake wembamba nao wana namna yao hadi kufikia kilele
-       Na wale wa umbo la kati wana jinsi yao ili kufikia kilele

Katika KI-TUTA hiki – ambacho ni kumaliza mtihana wa chekechea ya ndoa na kuingia PRIMARY SCHOOL ya ndoa; darasa kamili la Primary. Huwa ni hili la KUVUMILIANA na KUCHUKULIANA na lengo lake ni wanandoa wote kupata UJUZI, UZOEFU na USTADI katika maisha ya ndoa yao.

Wapo wengi wanaokaa katika darasa la chekechea hata kwa miaka hadi 50 ya ndoa kama hawana walimu wa kuwatoa katika ujinga wao. Lakini wengine ni muda mfupi tu wanakuwa wamefauulu na kuvuka darasa hili kwa sababu ni  WANYENYEKEVU, WAKO TAYARI KUJIFUNZA na WAMEFUNDISHWA NA MWALIMU MZOEFU.

KITUTA CHA PILI
Baada ya wanandoa hawa kushinda mtihani wa chekechea na kuingia Primary, wakati huo wote wanakuwa kwenye darasa la kusoma na tabia na kuchukuliana na kuvumiliana.
Kuogopana bila kuambiana udhaifu wao wala makwazo yao wao kwa wao ni dalili za UTOTO katika ndoa.
Lakini muda unatimia wa kumaliza woga wa wanandoa kuogopana. Wanapata ujasiri wa kuambiana ukweli na wazi wazi matakwa yao, mmoja kwa wenziwe kwa unyenyekevu. (unyenyekevu unahitajika sana katika darasa hili)

Kwenye KITUTA  hiki, kunakuwa na mvutano mkubwa kwa maana kila mtu huonyesha ubinafsi wake ambao unadhihirisha TABIA yake HALISI kama alivyolelewa au kuzaliwa.
Mara nyingi hapa wanandoa, kila mmoja anadai tabia ya mwenzake ni mbaya; na kila mmoja anataka mapenzi yake au madai/matakwa yake yatendeke. Kuheshimiana na kujaliana kunakosekana sana hapa.

Wanandoa wanaopambana kwenye KITUTA hiki, wakikosa
  1. Unyenyekevu  Flp 2:3-5
  2. Kutangulizana Rum 12:10
  3. Kumwogopa Mungu
  4. Kujaliana na kuheshimiana
Ndipo unapoweza kuona mambo yafuatayo yakiwepo katika ndoa hiyo:-
i.               Magomvi yasiyokoma
ii.              Kuto-kuelewana na kiburi
iii.            Kupigana mara kwa mara
iv.            Kulaumiana na kutukanana
v.              Kuchukiana bila sababu za msingi
vi.            Kudharauliana wazi wazi

Hayo yote ni matokeo ya kufeli MTIHANI wa Primary. Nayo ikumbukwe kwamba “failures” wote wa Primary hawavikwi taji wala hawaruhusiwi /hakubaliwi kujiunga na masomo ya sekondari.
Lugha ya watu waliofeli mtihani wa Primary ya ndoa ni hii
Mimi sitaki Hiki: Mimi sipendi hili, Mimi sitaki hivyo, ni ubinafsi unatawala. Na kunakuwepo na maneno mengi ya kubishana na kuvutana

Aya zifuatazo zinaonyesha kama wanandoa hawa hawatafaulu mtihani wao watapatwa na mambo haya yafuatayo:-
  1. Mith 3;32 Watakuwa chukizo mbele za Bwana, kutokana na moyo wa UKAIDI. Utakuwa Chukizo kwa mwenzio wa ndoa.
  2. Mith 6:18 Wataanza kuwaziana mabaya, na kila mmoja atamuona mwenzake ni M-BAYA
  3. Zab. 37:8 Watakuwa wenye ghadhabu na hasira kila mmoja kwa mwenzake
  4. Efe 4:31 Watajiweka katika njia mbaya na kutaka kuwaziana maovu na kulipizana ovu kwa ovu
  5. Math 5:38-42 Jino kwa jino vikianza hata kufarakana na talaka zinakuwepo katika mtihani huu wa Primary maana mioyo hufarakana
  6. Ebr 12:14-16 Kama hawatashinda mtihani wao, shina la uchungu (bitterness) litachipuka na kuanza kuwasumbua wengi; na hap wengi hutiwa unajisi kwa ajii ya wanandoa hao.
NDOA INAJAA UCHUNGU DAIMA KWA KUSHINDWA MTIHANI WA PRIMARY YA NDOA

Watu wanaovuka KITUTA hiki, ndoa yao inajaa furaha na amani na upendo. Tena wanajifunza kusameheana na kuombeana pamoja na kuachiliana maovu yao.
Lazima UPOLE na MOYO WA KIASI viwe ndiyo maisha mapya ya wanandoa hawa. Gal 5:22-23
Ndoa yao inajaa mema na baraka iwapo watashinda mtihani wao
Zab 133;1-3; Zab 36:3
WATAANZA KUJIONEA BARAKA KATIKA NDOA YAO
Wapo wengine ambao baada ya kushindwa mtihani wa Primary ya ndoa, wanaishi katika kushindwa huku hata uzeeni. Lakini wengine huchukua muda mfupi tu na kutoka wakawa washindi. Watoto huwa wanaumia sana kuwakuta wazazi katika hali hii ya magomvi na kudharauliana. Watoto wanakosa amani. Nao huiga tabia mbaya kwa wazazi hata kama watakuja kuishi katika ndoa zao.
Majirani nao wanakosa amani na ninyi kwa maana mnakwaza watu kutokana na mwenendo wenu m-baya
MNAMTIA KRISTO AIBU
Ni lazima ushinde majaribio yote
Wengine kwa kushindwa huachana na kutengana bila kutaka suluhu
Wengine huamua kulipa baya kwa baya
Mpenzi mwanandoa, Usiuige ubaya bali uuige wema na Ushinde ubaya kwa wema 3Yoh 1:11

KITUTA CHA TATU (Secondary and High School
Kwa kumaliza kituta cha pili; unatembea katika njia ya kusameheana na kutafuta amani ya kweli. Kituta cha tatu ni cha MAAMUZI na MSIMAMO
KUAMUA:- Kudumu kuishi katika ndoa na kumcha Bwana au
Kukata tama na kuasi kwa kuamua kuishi katika uovu
Unafiki katika ndoa unaanza kuwa katika ndoa kwa ujanja na hila – kwa kuanza kutendeana maovu kwa siri au kwa wazi
Kufichana kudanganyana kusihi gizani. Ndoa ya kimwili; bali ki-moyo haipo
Hapa wanandoa wanatakiwa wanie mamoja na kutembea nuruni siku zote. Waishi maisha ya kweli na h aki mbele za Mungu
Wanaofeli mtihani wa Sekondari hawaingii chuo kikuu. Jitahidi ushinde. Re-sit kama ulishindwa ili ubalance credit.
Wanaoshinda mtihani huu huingia katika Chuo kikuu cha Mungu na kuanza shahada yao ya kwanza ya ndoa, yaani KUISHI KWA FURAHA SIKU ZOTE NA MWENZI WAKO
Kuipata shahada ya kwanza ya ndoa, ni gharama kubwa inayohitajika kwa wanandoa hawa, maana
  1. Mith 8:13 Kuchukia uovu. Na kumcha Bwana kuepuka uovu
  2. Mith 1:7 Mith 3:7, Mith 10:27 Kicho cha Bwana huongeza siku za kusihi kwa mtu
  3. Mhu 7:9 kuwa wapole bila kuonyeshana hasira
  4. Mith 3:33b Kutendeana kwa haki wao kwa wao
  5. Mith 4;14, 1pet 3:15 kujiepusha na njia ya wabaya na kuwa na mwenendo safi
  6. Zab 118:6-7 Kukaa upande wa Bwana
  7. Yer 17;7-8 Kumtegemea Bwana wote kwa pamoja katika mambo yao
CHUO KIKUU WATU NI WAZIMA, WANAJIHESHIMU, WANAJALIANA NI WAELEWA. Kuna Bachelors, Masters PhD nk za ndoa.

HITIMISHO (Summary)
KUSUDIENI KUMALIZA VIZURI MAISHA YENU YA NDOA KWA KUWA NA SIFA NJEMA
  1. Ndoa ni jambo la umilele na halitengwi na kitu chochote isipokuwa mauti peke yake
Rum 7:2-3 Jitahidini kuziba nyufa, msije mkajenga ukuta
  1. Ndoa ya Kikristo haina kuachana wala talaka. Mal 2:16 Mtu hana ruhusa kuitngua ndoa. Mungu akiunga mkoni kitu, Mwanadamu hana uwezo wa kukibatilisha. Labda kama anataka kufa Math 19;6 Jilindeni msiwe wazinzi. Mith 6:25-32
  2. Kaa na upange gharama zote za safari ya ndoa, kabla hujaianza na kufikiri na uamue kiusahihi kabla ya kuweka msingi LK. 14;28-29
  3. Wanandoa wasipomaliza mwendo wao vema na kuulinda ushirika wao, jambo hili huleta DHIHAKA  nyingi, FEDHEHA TELE, na MAUMIVU yasiyokoma kwa (2Tim. 4:7):-
  1. Watoto wenu mliowazaa
  2. Wazazi waliowazaa
  3. Jamaa na marafiki zenu wanaowazunguka
  4. Kanisa la Mungu au mwili wa Kristo
  1. Dumisheni Agano lenu. Kumbukeni kiapo chenu. Msisahaui upendo wenu wa kwanza. Pendo lenu lisiwe la kugeuka geuka. Mal 3:6, Ufu 2:4-5
KUENI – IWENI WATU WAZIMA. Ndoa zenu zikue, zikomae ziwe za kiutu uzima
  1. Safari ya wanandoa inahitaji ushindi wa kweli katika kila jaribu. Kushindwa katika eneo lolote hilo ni donda ndugu la ndoa yenu. Ni UKIMWI tena ni KANSA ya ndoa yenu Ufu 2;7, 11:17, 22-25 Ufu 3:12, 21. Ondoeni haya mambo katika ndoa zenu. Msikubali kushindwa. Kuishi maisha ya ushindi kila siku katika ndoa yenu ni NEEMA pekee toka Mungu; tena inahitaji wanandoa wanaomcha Mungu. Hakuna taji za walioshindwa mchezo
  2. NDOA IKIANZA NA MUNGU; NDOA HIYO IKIDUMU KATIKA KUMCHA MUNGU NA KUMHOFU; NDO HIYO ITAMALIZA MWENDO SALAMA NA KWA HESHIMA NA UTUKUFU MWINGI
Mungu huwawezesha wanandoa
  1. Wawe na upendo usiokinaika
  2. Wawe na furaha isiyoneneka kila mara
  3. Wawe na amani isiyo na ukomo
  4. Wawe na uvumilivu wenye matumaini
  5. Waishi kwa utu halisi kwa Ki-ungu
  6. Wafadhiliane bila kuchokana au kuhesabu mambaya
  7. Waaminiane na kuaminiwa na watu wote
  8. Kila mmoja wao anamhurumia mwenzi wake mna kumtendea mema. Ni wapole
  9. Akili zao zinajaa upendo na amani ya Ki-Mungu; wana kiasi, wanajizuia, wana nguvu hawashindwi au hawawezwi na jambo lolote
NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU Flp 4:13

Prepared by Rev. Imanuel E. Marandu
WEPEC
BOX 5435 DSM
MOBILE 0713 235199



SOMO   LA VIJANA :
KIJANA  UWE  MFANO  NA KIELEZO


Rum 12:1-2 TOA MWILI  WAKO  UWE DHABIBU
Kijana ni lazima ujue ya  kuwa  mwili wako  ni Hekalu  la mungu 1kor 3;16-17.
Kijana ajue ya kuwa ndani  yake roho wa mungu anatakwa  akae  -Mdo 2:17-21.
Kila kijana  akiutoa mwili ili Roho wa mungu amtawale –hay a yafuatayo ni lazima   atashinda
Atazishinda  tamaa za mwili –Gal 5:16
Atauweza mwili wake katika  utakatifu  na heshima- na hataishi katika  hali ya TAMAA MBAYA – 1Thess 4:3-5
Ataushinda ulimwengu maana ana nguvu 1Yoh 2:13-14
Ataishi maisha ya ushindi daima kama atausulubisha mwili wake pamoja na tama zake. Gal 5:24 na aishi kwa ajili ya Yesu –Gal 2:20
Kijana ujue ya kuwa wewe ni Taifa la Mungu – 1pet 2:9 ishi kama kijana – aliyezaliwa mara ya pili Binti wa kuhani Law 21:9 Usewe kahaba. Tendo la ndoa kwa watu ambao hawajaoana ni ukahaba. Jilinde usimwaibishe Baba yako kuhani kwa kufanya ukahaba – Mw 34:1-31 Dina Binti leah motto wa Israel akafanywa kahaba – akafanya ukahaba. Kukubali kushiriki na mtu mume au mtu mke kama si mke au mume wako huko ni kufanya ukahaba. Kujiliwaza na asiye wan do – bila ndoa ni ukahaba Mw 38:11- Yuda akalala na Tamani mkwewe akidhani ni kahaba – kahaba anapokea wengi na kulipwa.
Mkumbukeni Rahabu – Amosi 2:1 alikuwa kahaba usiwe kama Samsoni – alikuwa mnadhiri wa Mungu lakini – mwili ulimuweza – ukahaba ulimponza. Alichumbia akaanza kushiriki mambo yote kabla ya kufunga ndoa – Amuzi 16;4
Jilinde – usifanye upumbavu katika Israel ukafanya ukahaba ukiwa katika nyumba ya Baba yako. Kumb 22:21 Tunza ubikira wako ndani ya Yesu Kumb 22:15 Aliyeokoka ni kufanya ukahaba KIROHO. Tunza unyofu na usafi wa Kristo.

Kila jambo lin awakati wake – Mh 3:1-6 kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa kuna wakati wa uchumba na wakati wa NDOA – Uchumba si NDIOA usifanye hivyo usiwe mjinga.
Wewe ni hekalu la Mungu. Roho  wa Mungu anakaa ndani yako – 1 Kor 6:19 wewe si mali yako mwenyewe
Mwili wako uutoe  uwe sadaka kwa Mungu – Shetani hawezi kugusa sadaka ya Mungu
Rum 12:1 . Toa mwili wako uwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu. Kila mtu mwenye Roho wa mungu ndani yake ni Hekalu la Mungu – huyo ataushinda ulimwengu.
Mabinti mliookoka msiige mabinti wa duniani. Wao ni wa chini – sis ni wa juu. Wao ni wa hapa, sis ni wa kule. Wao mfalme wao ni Shetani – Sisi tuna Bwana Yesu yeye ndiye mfalume wetu. Wao ni  giza sis ni mwanga wa uzima – wao ni watumwa kila aliye wa ibilisi ni mtumwa wa dhambi na mshahara wake ni mauti
Usikubali kumwaibisha Yesu- usimpe ibilisi nafasi usimvunjie Kristo heshima- usikubali kuitwa kahaba utashinda – Jipe moyo – Yesu ni Bwana – utayaweza katika yeye akutiaye nguvu – Amen



UWE KIELELEZO KWA WAAMINIO
1Tim 4:11-12 Angalia mtu awaye yote asiudharau UJANA WAKO- BALI UWE KIELELEZO KWAO WAAMINIO
(i)             KATIKA USEMI WAKO
(ii)           KWA MWENENDO WAKO
(iii)          KATIKA UPENDO WAKO
(iv)          KATIKA KUAMINI KWAKO
(v)           NA KATIKA USAFI WA MOYO NA MAISHA YAKO

  1. KATIKA USEMI: Kor 4:6 Ujue jinsi ya kumjibu kila mtu – usiwe mwenye maneno ya ovyo. Mawazo yako yakolee munyu – ili upate kujua jinsi ya kuwajibu waliookoka, wayaudi wayunani, wazee, wabab wanaume vijana wa rika lako wadogo zako na kila mwingine mtu. Neno ovu lisitoke kinywani mwak Ef. 4:29, wala maneno ya upuuzi, wala maneno ya aibu Ef 5:4 wala matusi yasisikike kinywani mwako.

  1. KIJANA UWE KIELELEZO KWA MWENENDO WAKO

a)     Mwenendo wako kijana na uwe kama invyoipasa INJILI YA KRISTO flp 1;27
b)    Kijana UENENDE KAMA INAVYOUSTAHII WITO WAKO
-       Kwa unyenyekevu wote na upole Ef 4;2
-       Kwa uvumilivu na kuchukuliana katika upendo
c)     Tuenende kama watu wenye Hekima Ef 5:15-16 kijana uenende kwa hekima
d)    Kijana uenende kwa KUMPENDEZA MUNGU KABISA
-       Uzae matunda kwa kila kazi njema
-       Tena tuzidi katika maarifa ya Mungu
-       Usiwe kijana asiye na maendeleo – zidi - usipungue
e)     Kijana USIENENDE katika ufisadi na tama na karamu za ulafi na ibada zza sanamu 1Pet 4:3
f)     Kijana anatakiwa uwe na mwenendo kama ule wa Yesu – na aenende kama Yesu alivyoenenda 1 Yoh 2:6

  1. KIJANA UENENDE NA UPENDO 1 YOH 3:18
(i)             Uwe na upendo wa matendo si wa ulimi
(ii)           Uwe na upendo kama huu 1Kor 13:4-8 upendo wa Mungu wenye sifa zote
(iii)          Kumpenda Mungu kwa moyo wako wote ee kijana na roho, na moyo kwa nguvu zako zote na jirani kama nafsi yako mwenyewe
(iv)          Kijana awe amejaa pendo la  udugu na kwa heshima awatangulize wengine Rom 12:9-10
(v)           Amri ya Mungu kwa kijana mpendane Yoh 13:34
(vi)          Apendaye amezaliwa na Mungu.

  1. KIJANA AWE AMEJAA IMANI
(i)             Amwamini Mungu katika mambo yake yote Yer 17:7 Aaminiye Mk 9:23
(ii)           Kijana aishi si kwa wasiwasi bali kwa UHAKIKA aishi kijana mwenye TARAJA. Ebr 11:6 na kwa kuwa na imani – TUNAMPENDEZA MUNGU
(iii)          Kijana awe na imani TIMILIFU ya kung’oa MILIMA, 1Kor 13:2 Imani isiyo na upungufu Mt 17:20 Na imani yako iwe ni imani isiyoshindwa na jambo lolote
(iv)          Kijana awe na imani kwa yale unayombwomba Mungu – uwe mwenye Imani si mashaka mwenye Imani HUOMBA NA KUPOKEA mk11:20-24
(v)           Kijana imani yako iwe hai nafsini mwako. Onyesha imani yako kwa MATENDO si kwa maneno. Yk 2:18 kijana imani yako IZAE KAMILISHA IMANI YAKO KWA NJIA YA MATENDO USIWE NA IMANI PEKEE AMBAYO HAINA MATENDO. Ili imani iwe na manufaa ni lazima ichanganyike na neno la Mungu ndani yake Ebr 4;2 Mchanga ukichanganyika na Cement – kuna kitu kinachozaliwa, kinaonekana tofali au Zege. Imani ichanganywe na neno :- Kijana uwe na imani ambayo misingi yake iko ndani ya neno la Mungu. Imani bila neno la Mungu haina matokeo – haipo Rum 10;17
(vi)          Imani yako – kijana iwe ni imani kubwa Lk 7:9
(vii)        Kijana uwe na kiasi cha Imani – Rum 12:3 Usinie makuu kupita ikupasavyo kunai

  1. Kijana unatakiwa uwe na maisha yaliyo safi usiwe mchafu kiroho – uwe na Moyo safi Ebr 9:13 Ukiabudu maisha yako yawe yamesafishwa na DAMU ya Yesu. Kijana uwe na dhamiri safi mbele za Mungu Ebr 10:19-23 Kijana uwe na jibu la dhamiri safi mbele za Mungu. Mt 5:8 Ishi maisha yenye Uheri ee kijana – Uwezeshwe kumuona Mungu daima. Kijana – Mungu ni mwaminifu ndiye awezaye kukusafisha kabisa nafsi yako, roho yako na mwili wako uwe safi bila lawama hata siku ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo
-       Bila neno hakuna utakaso – bile neno- hakuna usafi Zab 119:9 Yoh 17:17- uwatakase kwa ile kweli – neno la mungu ni kweli. Yesu akasema “Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile  neno nililowaambia:-
-       Kijana ishi maisha mapya 2Kor 5:17 Ishi katika upya wa uzima – kijana usifuanane ulimwengu – kijana usigeuzwe na dunia bali uigeuze. Uifanye dunia ikufuate wewe. Kijana uwe mpya katika nia yako – kijana usinie ya ulimwengu huu kama mtu wa dunia hii.

SUMMARY
Kijana/binti usijifananishe na Bar maid katika mfano wako – usivae kama kahaba – kahaba huvaa anavyovyaa ili awavutie wale wanaomtaka au anaowataka Mw 38:14 mavazi yalimfanya Yuda akamdani mwali wake kuwa ni kahaba – akazini naye
Wateule wanavaa mavazi ya kujisitiri 1tim 2;9 si mavazi ya kujiachia uchi uchi. Mavazi hueleza kazi ya mtu – kama Nurse akipita – tunatambua kirahisi kwa mavazi yake. Polic traffic kwa mavazi yake mwanajeshi kwa mavazi yake rubani wa ndege kwa mvao wake je wewe unatambulika kwa jinsi gain?
Unaelezekaje? Fanyika upya leo – geuka leo- toa mwili wako uwe dhabihu leo. Mpendeze Mungu leo. Jua kuwa ni mapenzi ya Mungu uichukue sura ya Yesu Rum 8:29 Uwe na sura ya mbinguni ukiwa hapa duniani 1kor 15:48 -50 uishi kama mwana na Mungu na si kama mtu baki. Uonekane kama mwana wa Mfalme na si kama mtumwa – upande farasi wala usitembee kwa miguu Mh 10:9-10 uwe mtawala, uwe Kijana usikwaze wayahudi wala wayunani wala Kanisa la Mungu

Mungu awabariki sana



Prepared by
Rev. Immanuel E. Marandu Word Evangelism and Pentecostal Explosion Church
0713 235199/0754 681438
DAR ES SALAAM












SOMO LA NDOA
USIMLAUMU MWENZIO

  1. KUMBUKA ULIMPENDA MWENYEWE

UENDO: 1 Kor 13: 14 -8, Kol 3:12-17
(a) UPENDO – Huvumilia – kuvumilia nini?
    Rumi: 8:35 Mateso, shida, adha, dhiki,2 Kor 4:7-12: njaa, uchi hatari, Upanga
(b) Kukmbuka wewe ni chombo cha udongo.
(c)  Adhama kuu ya uwezo wako iwe ni kutoka kwa Mungu
(d) Usizitumaini akili zako mwenyewe Mith. 3:5-7.
(e) Mkiri Bwana mtamke Yesu sema neno la Mungu.
(f) Usiwe mwenye hekima (mjuaji) ukijiona wewe u sahihi kwa kila kitu
(g) mche Mungu mheshimu mwogope
NDOA NI MWILI MMOJA (si wawili ni mmoja)
  • INA MWILI: Mwili unahitajika uwe na afya –Mith 14 :30
  • INA MIFUPA: mifupa inahitaji mafuta 1 Yoh 2:27; je umeyapata mafuta hayo? Kama bado tafuta uyapate.
  • Ukiyapata halafu yakakaa ndani yako ’yatakufundisha habari za mambo yote elimu, kazi, Bishara, kilimo, ufugaji, ndoa kuhubiri,kuomba 8:26-27 Roma. Nk.
  • Taka sana ndoa yako iwe na neema Tito 2:11-12

  1. UPENDO HUFADHILI: Fadhila ni nini?
Anayefadhiliwa ni mtu wa namna gain? Ef. 4:32: Mfadhili Mumeo/Mfadhili    mkeo umhurumie, umsamehe.(anayesamehewa ni mtu wa namna gain?) 1 Kor 3:1-3 watu wa mwili.
  1. UPENDO HAUHUSUDU: Husuda ni nini? Je unayo?
Unamhusudu mkeo kwa vile ana kibali kuliko wewe? Unamhusudu kwa vile wanampenda kuliko wewe? Usifukie visima Mw 26:14-18 Husuda huziba vyanzo uhai wa kila kiumbe/kazi n.k. husuda hutenda jambo la kuangamiza (Mw. 26:12-20.
Mungu akujue (zab.19:13)
Mungu akuzuie na mambo ya kiburi tena uombe yasikutawale ..Utawala ni nini?
Enendeni kwa roho nanyi hamtazitimiza kamwe

-       Tamaa matakwa ya mwili gal :5:16,19,21 ifanye ndoa yako itawaliwe na  Mungu .Enenda kwa kuongozwa na Roho katika ndoa yako nawe utashinda ugomvi. Mith.21:9,19.
-       HASIRA mh.:7:9 hasira hukaa katika vifaa vya wapumbavu kaukaa/kuweka hasira: Mith 16:32, utakuwa mwema kuliko shujaa. uwe na uwezo wa kuitawala Roho yako 16:32
-       Uwe mwepesi kusikia lakini usiwe mshapu wa kusema, kujibu wala kukasirika. Yak 1: 19-20: wekeeni mbali hasira uchafu wote na ubaya uzidio.
-       Kol 3:8 weka hasira mbali nawe ( hasira huzaa ugomvi Ef. 4:26) penye ugomvi pana kila machafuko, matusi, kashfa.
-       Hasira ni chanzo cha kila tendo baya (kupigana) kwa hiyo mwnandoa wekea mbali nawe uovu wowote ule.
-       Uujuao ni uovu
-       Hila zote zile uzijuao ni hila
-       Unafiki wote ule uujuao ni unafiki.
-       Husuda zote zile uzijuao ni husuda.
-       Masingizio yote yale uyajuayo kwamba ni masingizio. Hasira ya Mwanadamu haitendi (haki, mema ya Muntgu) yak: 1:20 jilinde usimpe ibilisi nafasi Ef. 4:27.

4. UPENDO : HAUTAKABARI: Utakabari nini?
Ni kujiweka kwenye Cheo , Ngazi, Madaraka, Mamlaka, Uwezo ambao haujawekwa na mamlaka husika. 1fal 1:5 kama mke kumtawala mume, 1Tim 2:12 . kama maamuzi yanayopingana na agizo la Mumeo. EVA maamuzi yanayovunja amri za Mungu. Mw. 3:6: hata kama ni jambo linalopendeza machoni pako au linafaa angalia vizuri, usifanya maamuzi kiubabe bila kumshirikisha mume wako usifanya neno kwa kushindana. Flp 2:3 kwa majivuno au kiburi.

Yawezekana matatizo yaliyo katika ndoa yako ni wewe. U mume /mke mwenye kutakabari acha tabia yako hiyo ukawe mwanamke mpole mtulivu na mtii. Mambo yote yatarekebika usimlaumu mwenziwe, rekebisha leo/ badilika leo.

5. UPENDO HAUJIVUNI: Kujivuna au kujivunia ni kupi au ni kitu cha namna gain?
  • Kujidhamini wewe binafsi
  • Kujiona unafaa kuliko mumeo/mkeo
  • Kujikinai, kujiona mwenye haki kuliko mume/ mkeo .
  • Moyo, tabia ya kudharau wengine wote pamoja na mumeo/ mkeo.
Flp 2:3: Jihadhari usitende neno lolote kwa kiburi / kujivuna ili kushindana.
Kiburi huleta mashindano: Mith 13:10

Bali jitahidi fanya bidii, jihimize, jifunze,
a)     Kumuona mumeo/mkeo ni bora kuliko nafsi yako, usiwe mtu wa kujipendeza nafsi yako mwenyewe.
b)    Jifunze kutenda kazi/mambo/maneno yako kwa unyenyekevu. Unyenyekevu ni nini?
c)     Mwone mwenzio anastahili kuliko wee kwa msingi huu.:

1.     utauliza ushauri kwa mwenzio: Mith13:10
2.     utamheshimu mumeo/mkeo( hofu kwake)
3.     utamjali mumeo/mkeo kuliko unavyojijali binafsi.
4.     huamdharau wala hutamvunjia heshima mkeo/ mumeo, staha itatawala ndoa yenu.
Kujivunia huletwa  na kiungo kudogo katika mwili wako kiitwacho ulimi.
Ulimi            - Huwasha moto ndoa yote
Ulimi         - Huwasha moto mambo yote
ulimi            - Huwasha moto maumbile
Ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wanandoa kujilinda sana na matumizi ya Ulimi.
Kiungo Ulimi: Kama usipokitawala kitaweza kuleta mambo yafuatayo katika ndoa yako.
Kuzuia mafanikio yote ya ndoa yako.
  1. Kuzuia mafanikio yote ya ndoa yako.
  2. Kuleta makwazo ya kila namna katika ndoa yako
  3. Kugeuza ndoa yako ielekee kokote kule kama utakavyosema kama kuachana, kufarakana, kudharauliana.kwenda nje ya ndoa, kuchukiana.


Ulimi si kiungo cha kuachilia kinene tu kwani kila kinenwacho kwa kumaanisha kinatokea, aidha ni neno jema au baya LAANA au baraka ziko katika uwezo wa ulimi kila mtu atakula matunda ya ulimi wake utafakari leo umeinene ndoa yako mambo gain? Umenenea mumeo/mkeo mambo gain?

YAHARIBU: Mafaili hayo huko kuzimu kwani kila ovu utakalonena, kuna pepo ameamriwa alifuatilie na aiahakikishe limetekelezwa kuna kumbukumbu, kuna faili kuzimu. Ndio maana unaweza kuona wateule wengine wakipatwa na mabaya, kumbe waliwahi kujinenea wakasahau. Omba Roho Mtakatifu Akukumbushe, akupe toba ya kweli, uyafute kwa kuyanenea baraka / mema-badilisha, bado hujachelewa”. Kila jambo lina wakati wake na kila kusudi chini ya mbingu lina wakati muafaka wa kulitenda. Mh. 3:1.

Huhu ni wakati uliokubalika kwako kurekebisha kubadilisha / kusahihisha / kuiweka kwenye njia sahihi ndoa yako hadi ifikie HATMA njema.  Uzima au mauti viko katika uwezo wa ulimi.  Letea ndoa yako uzima tena kwa kuinenea kwa ulimi wako. ‘Mith. 15:4’ pokea uwezo wa kunena pokea hekima unene mema ili yapate kukujilia.  Fikiri kabla hujanena.

Acha ushupavu Mith 16:28 maana kwa huo moyo wa ushupavu umeshapata unasababisha fitina kuanza, ulimi wako wanena maneno.  Epuka maneno ya kukushupaza Mith. 18:6. Ndoa yako umeiletea madhara kwa sababu ya ushupavu wako. Uwe milaini, mnyofu.  Mshupavu, anavunjika shingo yake ghafla na hana tabibu wa kumtibu Mith. 29.1; Hana dawa. 

Mshupavu ni mtu asiyeshaurika mume/mke asiyepokea maelekezo yoyote. Kwa moyo wake hakubali kugeuzwa hata akishauriwa utaweza ukamsikia akisema, “pamoja na ushauri wake mimi msimamo wangu ni ule ule, sikubali mtu anitendee hili.  Si mimi wa kuchezea hanijui tu’ maneno yanayoumba matendo ya ukaidi milima ya kiburi na kusababisha FITINA- NI MAPINDUZI. Mtu mwingine kukuondokea akachukua nafasi yako ya utawala.  Mke akiwa na moyo wa ushupavu, hashauriki haelekezi na king’anganizi, kibabe mke au kijike dume.

FITINA: pepo anamwandaa mwanamke Fulani ainue fitina/mapinduzi amchukie mume/mke. 2Falme 11:13-14 Umestukia mumeo katekwa n amwanamke Fulani-yuko naye-yawezekana na NDIYO ulivyo- MSHUPAVU – Hushauriki kauli zako ndio hizi:- UTANIFANYA NINI?  Ndiyo lugha yako “Nimezoea kuvaa hivi nyumbani ukiwa NADHIFU – smati – MSAFI – Una nywele zimekaa sawa na ni safi – inampa mumeo kuona kwamba unamjali/ unamheshimu.  Kuwa hivyo kunamvutia mumeo akufurahie na akupende kuliko kawaida.

LABDA MUMEO anataka uvae nguo za aina Fulani – na sio matene ya kujisokotea au vigauni vya (kibar maid) wauza bar na hafurahishwi na mitindo ya aina Fulani ya mivao – USHARIBU NDOA YAKO KIJINGA YA AWEZEKANA HII NDIYO TABIA YAKO- Unapenda uwe kama mama Fulani – uvae kama dada Fulani- utasababisha fitina kwa USHUPAVU wako huo na kusema sema, “usiniingilie – ndio napenda mie hivi Mbona mama Fulani anavaa – mbona mumewe hamuulizi – we vipi – usiniletee ushamba wako – Hujanioa unitawale – chukua time mi si mtu wa kuendeshwa kama gari bovu – kwangu sibadilishi ng’o” (Mafarakano huanzia hapo) kwa kauli hizo kiumwamba- zisizo na adabu wala nidhamu  UMEMWINGIZA IBILISI WA FARAKA KATIKA NDOA YAKO.

Kumbuka Mith 16:28b Mkifarakana kwa ajili ya ushupavu mume anaanza kumteta mke wake kwa watu.  Mke anamteta mume wake kwao au popote pole kinachofuata ni tunda la ushupavu wako MARAFIKI WALIOAMBATANA yaani WANANDOA  wafarakane – watengane – waachane – watalikiane MPENZI MPENDEZE MUMEO/MKEO 1Kor 7:32-32 Aliyeolewa asitafute ajipendeze; bali ampendezwe YEYE bali ATAFUTE jinsi ya KUMPENDEZA ALIYEMWOA. USIJIFANYE RAIS WAKATI WEWE NI WAZIRI USIJITIE UMANAGER WAKATI WEWENI MESENJA au AFISA MIPANGO SIMAMIA NAFASI YAKO.  Dumisha NDOA YAKO ACHA MARA MOJA Maneno ya kiubabe/kiumwamba/kishupavu.

Kumbuka anguko lisilotanguliwa na kiburi – mkumbuke saddam Husein mkumbuke Malkia Vashti – Esta 1:1-28 Mith 1:18.

Kumbuka:
a)     Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake (usiwe mpumbavu) Mith 18:7 Mith 11:13.
b)    Nni midomo ya mpumbavu itaingiza wewe katika FITINA – USIKUBALI
c)     Kinywa chako kinaita mapigo- 18:1 Mith KIZUIE
d)    ZUIA ulimi uwe mtu wenye maarifa 17:27 Mith
e)     Kumbuka UKAIDI UNAZUIA MEMA 17:20 epuka kuwa na ULIMI ULIOPOTOKA.
f)     Kinywa chako kitakupa bidii 16:26 Mith.
g)     Usichimbie shimo ndoa yako wala usiitie moto – kwa ulimi wako Yak 3:4-11, Mith 16:27 mkumbuke Nabali 1Sam 25:1-30 mtu asiyefaa kitu/mkumbuke Mikali binti mfalme Sauli – alivyopigwa kwa UTASA -  Soma

6. UPENDO: HAUKOSI KUWA na ADABU
  Mahali ambako hakuna upendo haipo. Mith 11 :16

Mwanamke wa ADABU HUHESIMIWA DAIMA mwenye adabu anajali mumewe.  Mume mwenye adabu anamjali mkewae kumbuka mwanaume yule Nabali hakuwa na adabu. Adabu nzuri ni pambo la mwanamke kwa mume wake-1Tim2;9-11; Pambo zuri kuliko Hereni ya dhahabu au vikuku tena inazidi mapambo mengineyo yote. Wapeni watu haki zao. Rumi.13:7- astahiliye heshima  -apewe heshima- astahiliye KUPENDWA- AONYESHWE UPENDO- ASTAHILIYE HOFU? MUME USIMCHUKIE MKE/MKE USIMDHARAU MUMEO. Ef. 5:25-32, Ef: 5:22-24.

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE. Ebr.13:4- MWANANDOA- hakuna mtu atakayekusudia kumpenda mkeo/ wala hakuna wa kukusaidia kumheshimu mume wako. Wajibika acha uzembbe acha ujinga KUKOSA HESHIMA KULIKUFANYA UACHWE  kimyakimya.

  1. UPENDO: HAUTAFUTI MAMBO YAKE WENYEWE..
Hakuna ubinafsi. Kuna kumjali mwenzio 1Kor 7:2-5 kwanza Flp 2;3-5 kumthamini mwenzio. Kumbuka usiwe MBINAFSI KATIKA TENDO LA NDOA

USITAFUTE tu mambo yako mwenyewe- mpe mkeo haki yake – usimpunje katika jambo hili nawe mume usiangalie furaha yako mwenyewe, pia mke mpe mumeo haki yake- usiwe mbinafsi wa kumwekea masharti mengi. Mweleze akuambie atakachotaka kwako mwambie awe wazi ili umpatie haki yake. Ambianeni UKWELI MSIFICHANE- MNAPENDANA. Ebu tafakari haya yafuatayo na Mungu sana namna gain kuhusu yule mume/mke. ULIMPENDA/AKAKUPENDA MKAOANA NA sasa ni mume na mke wkao kwamba kwa nini mambo kama haya yapo katika NDOA YAKO SASA – na MSINGI wa ndoa yako ulianza na UPENDO; Mw 29:18-20, Wimbo 8;6-7 mbona lengo linasimama kama msingi haujaharibiwa Zab 11;3-4 ufa wa jingo ni kosa la MSINGI kumbuka Upendo: una nguvu kama (mauti) Mungu haushindwi unapazimia jambo.

USHUPAVU HULETA MVUTANO:- Malumbano mabishano yasiyokoma AZIMU-KUMPENDA – USIMJIBU MPUMBAVU sawa na UPUMBAVU wake ANAYEMCHUKIA MUME WAKE NI MPUMBAVU. Anamchukia mkewe na kugeukia wengine ni mpumbavu.  Anajichukia mwenyewe anachukia maisha yake, anauchukia mwili wake, anachukia mafanikio yake anayachukia mema yote ambayo yangepaswa yamjie, Ef. 5:26-32.

Mungu ni mwamuzi na mwangalizi wa KILA NDOA, na ni mtetezi wake. Malaki 2:15-20 jihadhari na mke au mume wa mwingine – MHESIMU MKE/MUME wako –USIZINI. Mw. 20:1-13 utakuwa MFU.  Ukiingilia ndoa ya mtu kumbuka Daudi na mke wa Uria – 1Sam 12:11-24 kuingilia ndoa ya mtu ni kumdharau Bwana.  Utavunjiwa heshima milele – mpaka kaburini mwako. Mith 6:27-33 HESHIMU MUME/MKE WA MWENZIO. Haya naye uyajue kuhusus yule ULIYEMPENDA – AKAKUOA/UKAMWOA. Je una mambo kama haya yafuatayo?

  1. ULIYEMPENDA: Hutaona uchungu kwa ajili yake Ebr. 12:14-18 hutasababisha shina la uchung kuchipuka – wala hutapenda apate UCHUNGU Ef. 4:31. Uchungu wote na makelele vindoke katika NDOA YANGU – MSAMEHEANE.
JE UNAYOFANYA YAMELETA HUZUNI NA UCHUNGU KWA MWENZIO? MWOMBE MSAMAHA KAENI MUONGEE.


  1. UNAYEMPENDA: hutamhesabia mabaya ina maana anaweza akawa nayo Mith 31:12 kuna wanaume wanawaona wake zao ni wabaya siku zote/ au wanaume zao niwaovu iku zote, wala haoni jema lolote kwa mke/wala mume wake.  Hawa ndio wanaohesabu mabaya HILI NI TATIZO LA NDOA YAKO – Acha hii tabia mara moja katika jina la Yesu. SIFIE HATA KAMA HIYO SI KAWAIDA YAKO – GEUKA LEO.


  1. UMPENDAYE: Akidhulumika hutafurahia udhalimu ni maovu – mambo mabaya yamempata mkme/mume wako nawe unashangilia kama umesikia duka limeibiwa nawe unashangilia, gari yake imegongwa unapiga na vigelegele.  Mungu hapendi, mke/mume si adui yako kumbuka ULIMPENDA UTALAANIWA NA BWANA MWENYE NDOA L.K 6:27-33 Mpende hata kama HAKUPENDI, mtendee mema hata kama anakutendea mabaya, usilipize kisasi MPENDE MUMEO MPENDE MKEO- Tenda mema ponya ndoa yako.  Adui wa ndoa yako ni wewe kuharibika kwa ndoa mume/mke wako ni WEWE. USIMSINGIZIE SHETANI – Ni wewe ulimwingiza ukampa nafasi Ef. 4:27 kwa mabaya kuliko kawaida. Yako na mema yatakuijia ZAb. 133 yote.  Furahia na kweli tu. TAFAKARI HAYA YAFUATAYO KISHA UKIULIZE  unayaweza? Filip 4:13.

  1. kwa kuwa ULIMPENDA UTAVUMILIA yote Yak. 1:24 Yk. 5-7

  1. Aminiyote kwa kumtanguliza Bwana upendo huamini yote unaaweza.

  1. Tumaini yote – upendo unaweza Rumi 5:2-5 soma kifungu hiki.

  1. Stahimili yote- Upendo una nguvu utakuwa na heri UKISTAHIMILI Yk 1:12. mwenye upendo hatapungua neno hata moja wakati wowote iwe ni wakati war aha au shida au mateso au adha/upendo unashinda Usisingizie shida au njaa.  Injulikana kama ni pendo katika vipimo. Asiyependa hatokani na Mungu anayemchukia mke/mume wake ni muuaji.  Na hakuna muuaji mwenye urithi katika ufalme wa Mungu UMEUA NDOA YAKO MWENYEWE LEO IFUFUE, WAJIBIKA MWENYEWE.


HAKUNA MWANADAMU ALIYEKAMILIKA  ila sehemu tu. USIMLAUMU MWENZIO WEWE NI MTU Hes 23:19

               i.         NDOA SI MCHEZO, kwamba tukubaliane na matokeo yoyote yale. Usikate tama.
              ii.         Hakuna ndoa iliyopangiwa kushindwa SHIKA AHADI HII UTOKE MSHINDILEO.
            iii.         Shetani hawezi kuifarakanisha ndoa ACHA MABAYA UKATENDE MEMA- utakubaliwa.
            iv.         Mwanadamu tu ndiye anayejaribu kutenganisha kile alichounganisha Mungu.
              v.         Mume ni wa mtu mmoja (mke) na si kw aajili ya wake wengi. NA MKE NAYE SI WA BOMA AU UKOO NI WA MUME MMOJA TU.
            vi.         Mungu hajapanga ndoa yako kuvunjia usikate tama amini tu itarudi.
           vii.         Umeharibu mwenyewe, tengeneza mwenyewe. Tengeneza mwenendo wako Zab 50:15,23 soma.
         viii.         Hukumu ya kuharibu ndoa ni kutupwa motoni au Jehanam.
             ix.         Talaka ni mpango wa watu umetoka kwa watu wala si kutoka juu.
              x.         Kwanini ushindwe? Wewe ni mshindi nayaweza mambo yote katika yey anitiaye nguvu flp. 4:13.

Na katika mambo yote UTASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA MAANA YESU ANAKUPENDA, Rumi 8:35-39. USIAMUE KUSHINWA – JIPE MOYO 1Kor 15:57

Neema na amani ya bwana wetu Yesu Kristo ikae na ndoa yako tangu sasa na hata milele. Amina.
Nawatakia baraka za Mungu na mafanikio mema katika. Ndoa zenu, siku zote za maisha yenu. Mungu awabariki.
……………………………….
Rev. Immanuel E. Marandu.
World Evangelism and Pentecostal
Explosion Church P.O. Box 45354,Dar es Salaam
Tel:0713 235199/0754 681438





























SOMO LA VIJANA
UTAJIPATIA HATIA
KUOA AU KUOLEWA ISIVYOSTAHILI :-1 Kor 11:23-26

Kuoa au kuolewa isivyostahili ina maana ya kijana au binti anayeolewa na bila kufundishwa maana ya NDOA na bila kuelimishwa jinsi ya kuishi na mume wake au mke wake katika ndoa siku zote za maisha yao.
Ndoa ambayo kijana au binti anaeolewa bila kupewa MAFUNZO yeyote yale au maisha ya NDOA ni sawa na :-
  1. Kumpa  mtu cheti na huku hajasomea taaluma ile inayohusiana na cheti hicho.
  2. Ni sawa  na kumwajiri  daktari ambaye hajasomea kazi ile, bali siku ya siku mlimfanyia graduation na kumvika majoho bila kuingia CHUO, wala kufanya MTIHANI wa HAJASTAHILI kupewa daraja hilo.
  3. Ni kumpa mtu (kijana/binti) cheo au wadhifa asiopaswa kuwa nao kama Ashari unampa combat na silaha na kumwingiza kwenye uwanja wa vita-bila kumfunza mbinu za vita.
  4. Ni kama kumvika mwanamichezo kama mpira wa miguu au net ball bila kupitia katika mikono ya kocha apate mafunzo na kila kifaa cha mchezo bila elimu ya kutumia vitu hivyo- bila mazoea navyo:- unamwingiza katika uwanja wa mashindano.
  5. Ni kama kumpa mtu kazi ya udereva /urubani/unahodha wa meli, gari au ngede bila kuwa na ujuzi wa kutumia vyombo hivyo:- unamkabidhi chombo na unampa idea kidogo jinsi ya kuanza mwendo na kwenda mbele_ lakini ujuzi mwingine zaidi ya pale hana. Hebu jiulize kama ni wewe. Hebu fikiri nikupe urubani _nikukabidhi ndege, nikupe utangulizi na namna ya kuruka je ukitaka kuigeuza huko angani utfanyaje? Je ukitaka kuifanya itue tena uwanjani utafanyaje? Je ramani au dira ya kule uendako –unaiweza? Je umbali wake na jinsi ya kufika huko unazijua? Je mafuta katika chombo chako yanatosha au vipi? Je wayajua matatizo ya anga? Kama upepo , mawingu mazito_dhoruba au radi??
2 .      Hebu ujiulize tumekupa wadhifa wa kuwa daktari – tukakuvika mavazi8 ya kidaktari na kukupa vifaa vyote vipasavyo na taaluma hiyo. Madawa yote na Phamacy na kila ofisi tukakukabidhi. Je wagonjwa sasa wameanza kuja kwako – na wanataka uwatibu- Je utawaandikia dawa gain kulingana na magonjwa yao??

=   Nahisi  hutajionyesha kushidwa na kwa kuwa unaijua- Asprin, Panadol na          Paracetamol, nadhani – kadi za wagonjwa wote zingejaa majina ya dawa hizi. Lakini si kweli kwamba kila ugonjwa dawa yake ni Asp Para au Panadol.
=  Hebu fikiri kama ni wewe nikupe jezi za wanasokoa – mpira wa miguu hujapewa zoezi hata siku moja- uangalie hili nalo- Nakupa wadhifa wa kuwa manager bila kukufunza uongozi – wadhifa wa kuwa MHASIBU bila kujua mahesabu ya kampuni hiyo yanawekwaje?
Mhasibu bila uhasibu – si mhasibu,- Rubani bila urubani si Rubani , Mwanamichezo bila mafunzo na mazoezi?? Daktari bila udaktari si daktari- . Ndoa bila elimu ni Ndoano. Ni kfo tu. Ndoa nyingi zimekuwa za shida mno mno kwa sababu _ Ni wajinga wawili waliopewa wadhifa  katika siku moja kuanza safari ambayo katika hiyo hakuna ajuaye aendako wala ujuzi wa njia hawana.
Watu wamediriki kusema _ Ndoa ni mateso , Ndoa na pingu za maisha, ndoa ni taabu tupu, ni msiba. Je kuna kusudi au mpango wowote wa Mungu wenye majuto ndani yake? Rum 11: 29
“Karama za Mungu hazina majuto wala mwito wake” Ndoa ni karama ya Mungu –Ndoa haina majuto-wala wale walioitwa kuingia katika jambo hilo hawana majuto-wala maumivu. Kama wanamtii yule aliyewaita na kukaa kama iwapasavyo katika ndoa zao.  Kila kitu ili kifanyikiwe, kuendelea, kiwe na faida ni lazima kutendwe kwa Akili na maarifa n juzi.
Ndoa ili ziwe nzuri – watu waishi kwa furaha, kla mume  amfurahie mkewe, kila mke aone raha na mume wake.  Tafuteni sana elimu ya ndoa kabla ya kufunga ndoaq na kumua mwenzio kabla ya kuishi naye  pamoja.
3. Somo lifuatalo linaeleza juu ya:-
          I.     . Umuhimu wa kumjifunza mume/mke wako mtarajiwa –umjue tabia yake mwenendo wake/ uzalendo wake, kiroho chake na uchumi wake kabla hamjaamua kuanza maisha ya pamoja.
        II.     Katik darasa hili utaelezwa faida za kukaa muda wa kutosha katika darasa la kumjifunza mwenzi wako wa maisha kabla ya kuoana naye.
      III.     Utaona kwamba- kuna mambo ambayo huwezi kuyabadili katika maisha ya mume/mke wako mtarajiwa. Lakini unaweza kuchukiliana naye kama alivyo bila kukwazika.
      IV.     Unaweza kupat nafasi ya kumshuri na kumgeuza au kumkarabati katika mambo mbali mbali – kama tabia,mwenendo, uzalendo wake, kabla ya kuanza kusihi naye.
        V.     Mume/mke unayemjua sawa sawa hawezi kukupa shida wakati wowote wa uhai wenu- kwani UNAMJUA na ulimjua kabla. Umejifunza kumchukulia.
      VI.     Katika somo hili- utapawe dondozi 9za utafiti wa kisaikolojia jinsi ya kumtafiti mwenzio na kumjua undani wake- kwa msaada wa najibu ya visairi vilivyotolewa kaufunguo wa utafiti huo.
    VII.     Pia – katika somo hili utapata kujua hasara za kufanya jambo bila kuwa na muafaka wa watu husika; na pia kutokwenda na wakati.
  VIII.     Utapata kuona faida za kutenda jambo kwa wakati ufaao na baraka za Mungu katika kulifuata neon la Mungu katika swala zima la kuwa Ndoa nzuri.
      IX.     Utajua nafasi ya wazazi/kanisa//jamaa au jamii katika ndoa yako.
        X.     Utafanikiwa kuwa na Ndoa yenye mwisho wa uheri – kwani umeanza na Mungu akubariki. Umche YEYE
4. Mabinti na vijana wa kiume ebu uwe mnyenyekevu – usome kwa uangalifu kijarida wa moyo wa kujifunza. Elewa vizuri kwamba kama ukiwa umepewa ramani ya kule uendako – hata kama ukiambiwa uende – utakuwa na – ujasiri maana una ramani – na unajua kule uendako:- Kumbuka watu wa mashindano yoyote wanaipitia ramani ya kule watakakopitia – kabla ya siku ya  siku ya mashindano.
Kumbuka: Daktari hufanya mazoezi mengi na mitihani mingi ya kidaktari kabla ya kupewa shahada – hufanya zoezi na chombo kile chini ya uangalizi wa  mwalimu/ engineer/ professor wake – kabla ya kukabidhiwa rasmi chombo chenyewe aendeshe mwenyewe. Wakati wa Uchumba ni wakati wa mafunzo/chuo/kozi malumu inayohusus NDOA unayoiendea.  Sasa – Uchumba wa leo? Umekuwa ni uchumba bila somo lolote.  Vijana na mabinti wanageuka kuwa makahaba kabla ya siku kufika. TENDO LA NDOA KWA VIJANA AMBAO HAWAJARUHUSIWA NA MAMLAKA HUSIKA (WALEZI /WAZAZI/KANISA) ni UKAHABA. Kumb. 22: 20-22 Law 21: 9  Vijana wengi leo, sio waliookoka tu, ila ni wote kwa ujumla – ambao hawana mafunzo – wamegeuka kuwa makahaba. Hata wengine wakafikia kupata mambi, na kufunga ndoa wakiwa wajawazito. Wengine baada au ufuska wa muda mrefu wanachokana na kutengan – Mabinti wengi wana kilio hicho. Kaka mmoja kamuacha na kwenda kwa binti mwingine.  Nimeona haya kwa muda mrefu kama yapata miaka37 tangu sasa nikiwa katika maisha yangu ya wokovu.  Mwanangu mpenzi – pokea hekima kami,li umshike Elimu maana yeye ni uzima wako – usimwache aende zake maana atakupatia taji ya uzuri na kukupa HESIMA- UKIMKUMBATIA. Atakupa NEEMA  kuwa kilemba KICHWANI PAKO Mith 4 : 5-9
5. Mwanangu mpenzi/ Binti/Kijana wa kiume mimi mwandishi wa jarida hili, nimekuwa kijana – kabla yako.  Nili[pompokea Yesu – nilikaa miaka 10 ya ujan nikiwa peke yangu bila mke.  Kitu cha kunishangaza ni kwamba enzi zetu- Kanisa/Wachungaji/ wazee – walitulea kuchapa injili tu na kutupeleka Bible School ili tuwe wainjilisti na wachungaji lakini la kushangaza sikuwahi kuona vijana kama vijana peke yetu tukikusanywa kanisani na kupewa mafunzo rasmi juu ya jambo hili la kuoa/kuolewa.  Sikuwahi kusikia popote semina ya vijana. Wala penginepo kuona jambo hhilo linatiliwa maanani sana, wala mkazo kuhusu maisha ya kijana na ndoa yake.  Mimi nilikuwa si mvivu wala mlegevu wa kuhudhuria mikutano waka makongamano lakini somo hili kwa upana sikulipata.  Nilipowaza kuoa mwaka1972, Mchungaji wangu (ambaye sasa ni marehemu) aliniambia neno moja tu, na bado sijalisahau:- nalo ni hili. “kijana wangu – ukimchumbia msichana akakukataa, usihuzunike kwani yawezekana, kama mngeoana ndoa yenu ingekuwa na matatizo”  La zaidi ya hilo sikuambiwa ila tuliambiwa kama Binti akikubaliana nawe – mje wote kwa Mchungaji kasha mtambulike kwa wazazi na itangazwe kanisani ili kama mtu mwingine akija asikuchumbie tena kwani una mchumba/umechumbiwa? Niliyoyapata ni haya yafuatayo:-
          I.     Ndoa zenye magomvi na kuchokana muda mfupi tu mara baada ya Arusi.
        II.     Ndoa zilizofungwa wanandoa wakiwa wana mimba.
      III.     Wanandoa waliofunga ndoa bila kujua kuwa kuna mambo mengine zaidi ya tendo la ndoa
      IV.     Wanandoa waliofungiwa ndoa, Binti hana habari kabisa kwamba kuna tendo la ndoa.(Hii ilitokea katika mji fulani mpaka wasimamizi wa ndoa wakalazimika kumkamata Binti huyo miguu – huyu mikono ndipo Bwana arusi akanza huduma yake) angalia ujinga kama huu.
        V.     Iliwahi kutokea kijana wa kiume kumkataa binti na huku ndoa imefungwa eti anaona ni dhambi jambo hilo.  Dada anambembeleza. Kaka anamkimbia huko ndani.
      VI.     Niliona na kuona watu wanaoana wala hawajui haki ya tendo la ndoa.  Ni wajinga na wabinafsi kila mtu hajui haki ya mwenzake.
    VII.     Nimekutana na Maarusi wasiojua kuheshimu jamii na jamaa – wala hawana adabu kwa wazazi wao. Wanabagua wazazi/wanapendelea wa kwao hata miradi yao au kazi kila mtu hana ushirika na mwenzake.
  VIII.     Nimeona ndoa zinavyovunjia kwa urahisi kwa ajili ya matatizo madogo sana – km dada yako hanitaki, wazazi wangu hawakupendi, hatuna mtoto. Amenitukana mume wangu/ hana kitu huyu, haniviki nguo, ameoa mwingine n.k.  Matatizo haya yote yanaweza kuepukika kama mtu akiolewa au kuoa akiwa na habati juu ya vitu kama hivi na njisi ya kuepukana navyo.  Kumbuka kinga ni bora kuliko kutibu.  Pia heri kuzuia uza kuliko kuzibaufa.  Bila maonyo watu hupigwa – hupata mateso, hutaabika – lakini wakionyeka hawatajuta wala kuteswa kwa jambo lolote lile.

NILIYOYAONA MWENYEWE
Mara nyingi niligundua makosa niliyokuwa natenda kuanzia uchumba wangu hadi kuoa nay ale niliyoyakuta katika ndoa yangu tangu 1979 hadi leo; nikaona ni mambo ambayo ningalikuwa nimepewa semina na mafunzo ya kutosha nisingeboronga kiwango kile au kiwango hicgho.  Sitaki huu msemo wa kusema
  1. tunajifunza kwa makosa – bali kujifunza kwa makosa ni kiwa watu wajinga ambao hawana mafunzo. Huu si wakati wa kuajiri walimu wasio na ujuzi. Na si muda wa kuwa na ndoa za WAJINGA NA WAPUMBAVU.
Hatutaki kuona taabu hii tuliyonayo sasa, ambayo ndoa mpaka za Masskofu na Wachungaji zina matatizo mazito sana.  Sina muda tena wa kuwa hakimu wa kusuhisha kesi za ndoa makanisani bali ili kuepuka kuendeleza ubovu wa ndoa katika kanisa la Mungu au katika Taifa au jamii.
II Nimeonelea niwatie moyo wachungaji wengi kufanya hivyo katika maeneno yao ili     kuliweka kanisa katika hali iliyo nzuri ya Ndoa bora na maisha mazuri yenye mfano wa   kuigwa na vijana makanisani.
III. Kuepusha ukahaba ndani ya kanisa na kufunga ndoa za WAJINGA
IV. sambamba na kwamba sasa napiga ndege wawili kwa jiwe moja – semina za wanandoa wa zamani najishunghulisha sana nazo ili angalau wakongwe HAWA
  1. Mume na mke waweze kuufikia mwisho mwema wa ndoa yao. Bila kuchokana wala kuoneana uchungu.
  2. Ukarabati wa ndoa utawafanya mume/mke wapendane tena kama kwanza –na kuheshimiana katika ndoa yao.
  3. Mume/mke – wafurahie tena tendo la ndoa kama wameoana leo – kwani ndoa haizeeki.
  4. Wajue kulea ndoa changa katika makanisa yao na kulea vijana na mabinti katika njia njema.
  5. Kujua jinsi ya kulea watoto na kuwaandaa kwa maisha yao ya baadaye waweze.
  6. Kusimamia ndoa na kuwa walimu kwa wanandoa wapya katika kutoa mafunzo kwao. (Table &Kitchen party).
PENDEKEZO KWA VIJANA WA KIUME


  1. Kijana wa kiume ni lazima awe na mafunzo maalumu ya kuingia katika ndoa kabla ya kufungiwa ndoa yake.
  2. mafunzo hayo yasiendeshwe na mshenga wa Arusi, wala mtu wa hivi hivi tu, bali ya kuwaasa vijana wa kime kwa maadili ya ndoa.
  3. si kweli kuwa wavulana wanajua na hawana haja ya kufundishwa na mtu.
  4. mfalme ni lazima aandaliwe vema ajue kutawala vema.  Mfalme mzuri anaandiliwa.  Ndoa njema inaandiliwa.

PENDEKEZO KWA MABINTI



  1. Binti apewe darasa la kuwa mke wa mtu kabla yakukabidhiwa ofisi yake – darasa hilo liendeshwe na mama mwenye sifa nzuri katika Ndoa yake au mwalimu rasmi aliyeandaliwa kwa kazi za nyumbani mwake.
  2. kitchen party isiwe ni kukusanya masufuria na miiko tu, uwepo muda wa kutosha jinsi ya kukaa na mume – na kutenda kazi za nyumbani mwake
  3. malkia huyu ni lazima atayarishwe kwa muda mrefu awe kamili na mmaknini kwa kazi za nyumbani mwake.
  4. Mke mwema – huandaliwa hatokei tu – hulelewa –Nyumba njema huandaliwa.

USIJIFANANISH NA WALIMWENGU
HAKUNA KWENDA NA DUNIA

MIMI N MWANA WA MFALME

RUMI 12:1-2 TIM. 4:11-12
1.     KIJANA ULIZALIWA MARA YA PILI USIJISAHAU, USIJIDHARAU, USIJIFANANISHE USIIGIZE, USIFUATISHE, AU KUJIFANYA KAMA KIJANA WA DUNIA.

Usijisahau:             kwamba wewe umeokoka
Usijidharau:            Unaweza kuish maisha ya ushindi – milele
Usijifananishe:  Wewe umes