Thursday, March 10, 2011

Stop Order!



Mchungaji Immanuel Elisa Marandu
Mimi ni Mchungaji Immanuel Elisa Marandu. Nimezaliwa Tanzania mkoa wa Kilimanjaro, wilaya ya Moshi vijijini, tarafa ya Vunjo kijiji cha Mandangeni Kirua Vunjo tarehe 19 mwezi wa 12 mwaka 1952 saa saba mchana siku ya Ijumaaa.
Nimeelimishwa elimu ya msingi shule ya N.A Pakula Kirua Vunjo. Mwaka 1961-1967
Nimempokea yesu mwezi desemba 1969. Nimebatizwa kwa maji mengi mwaka 1970 tarehe 15 mwezi Februari huko Old Moshi Shia.
Nimesoma Marangu bible school 1972 hadi 1973
Nimewekwa wakfu kwa kazi ya Mungu kanisa la FPCT Majengo Moshi tarehe 2 mwezi wa 9 mwaka 1973.
Nilihamia Tabora Mkinga wilaya ya Igunga mwezi Mei 1975, nilisomea ualimu toka 1976 mpaka Julai 1979 huko Tabora. Nilioa tarehe 6 Oktoba 1979. Nina watoto 6,
Betty, Vcky, John, Kefa, Nice na Sifaeli.
Mr and Mrs Rev Immanuel and Mary Marandu

Nilianza rasmi kazi ya mungu tena mwaka 1981 baada ya kumaliza bible school Pege Tabora.
Nilihamia Dar es Salaam Mei 31 mwaka 1991 kwa ajili ya kazi ya Mungu.
UDSM casfeta leaders.
UDSM casfeta fellowship 2011

              
Nina hudumia wanachuo na wanafunzi wa sekondari na high school hapa Dar es Salaam pia ninafundisha masomo maalum kwa:
Marangu TTC leaders.(Casfeta)2011.
Marangu TTC Ibada

1.Vijana ( Uchumba hadi ndoa)              
  2.Wana ndoa makanisa mbalimbali
 3.Crusade sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania
 4. Semina na makongamano ndani na nje ya Tanzani
5. Kuongoza vikundi vya maombezi ya kitaifa na kimataifa


Vi  Tumewahi kusimamia kambi ya maombi mlima Sakila kijiji Sakila wilaya Arumeru Arusha tangu 2005-2009 hadi serikali ya kijiji hicho ilipo vunja kambi hiyo kwa kuyaondoa mahema niliyo yaweka kwa ajili ya kuwakinga waombaji na mvua/jua na baridi ya usiku. Waliondoa mahema hayo tarehe 10 machi2009.
Kwa sasa ninaongoza timu ya maombezi ya kitaifa na kimataifa inayoitwa “Fathers Prayer Team”
1.     Team hiyo inajishughulisha kuombea kanisa la Mungu Tanzania na ulimwenguni.
2.     Taifa letu la Tanzania na mataifa.
3.     Uchumi wanchi yetu ya Tanzania na amani yake
4.     Uamsho ulimwenguni

Tuliwahi kufanya maombezi maalum tarehe 28 mwezi wa 5 mwaka 2010 hadi 31 mwezi wa 5 mwaka 2010. Tulifika hadi Uhuru Peak kuhitimisha maombezi hayo. Tulitumia siku tatu tu kwenda na Kurudi Marangu gate. Tulifika hadi uhuru peak kwa masaa 36:20 tu.
Tuna mpango wa kuwa na kituo cha kimataifa cha maombezi huko Arusha Ngaramtoni-Oloskito.  Eneo hilo lina ukubwa wa mita 70x70 bado hakija fanyiwa jambo lolote.Tuna hitaji watu wenye moyo na nia ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na Ulimwe ngu wajitolee kwa hali na mali kuendeleza kituo hicho kwa kutoa vitu vifuatavyo.
1.Mahema
2. Nondo
3 Cementi
4.Vifaa vinginevyo k.m Solar panel na solar lamps
5.Sim tank lita5000
6.Gari Hiace na Pickup
7.Matress-Nyembamba na sleeping bags.
Nifuraha yangu kama utawasiliana nami ili ujuwe lakufanya kwa ajili ya kambi hiyo ya Kitaifa na kimataifa ya maombi. Tunakukaribisha ushiriki Baraka hizi kwa kumtolea Mungu kwa ajili ya kambi hiyo ya maombi Arusha Oloskito.
Wasiliana nasi kwa simu namba
Pastor Lazarus Laiser +255 787 558668 +255 767 558668
Barua pepe lazarusls@yahoo.co.uk  Or
             Rev Immanuel Elisa Marandu +255 713235199 au +255 754 681458
Asante kwa kuwasiliana nami na kwa mchango wako Mungu akubariki!
Rev Immanuel E Marandu 11 March 2011.

MENGINEYO
1.Kwa yeyote anayetaka kujiunga na Fathers Prayer Team anakaribishwa sana.
2.Kutakuwepo na maombezi ya kuliombea taifa tena mwaka huu tarehe 28 Mei hadi tarehe 2 Juni 2011 mnakaribishwa kujiunga na kushiriki maombi na safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimnanjaro.
3.Kwa yeyote anayetaka kuchangia safari hiyo au kujiunga na Fathers Prayer Team tafadhali uwasiliane nasi kwa anwani zifuatazo:
rev.i.e.marandu@gmail.com au simu +255 713235199 au +255 754 681458
Mungu awabariki sana!
Reverend Marandu Kiwangwa Bagamoyo-Semina.
Reverend Marandu Kiwangwa Bagamoyo-Semina.
KIwangwa Bagamoyo Feb,2011
Rev I.E. Marandu.



Huduma Sehemu mbalimbali
Kiwangwa Crusade
Kiwangwa Crusade Feb,2011






Semina Kiwangwa ,Bagamoyo Feb, 2011






Reverend Marandu Kiwangwa Bagamoyo-Semina.




















No comments:

Post a Comment